Pole sana kwa msiba ulokufika!!
WAZIRI MKUU AFUNGWA JELA MIAKA 11
Mahakama Kuu ya Brazil imemhukumu kifungo cha miaka kumi na miezi 10 jela Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Jose Dirceu, ambaye ni katika watu wa karibu sana wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva, kwa makosa ya ubadhirifu na ufisadi.
Dirceu anakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya nafasi yake kununua kura za wabunge wa Brazil kwa faida ya chama cha mrengo wa kushoto cha Leba.
Taarifa zinasema kuwa, makosa yanayomkabili Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Brazil ni makubwa sana na ni pamoja na kutumia vibaya nguvu alizokuwa nazo serikalini, kufanya uhalifu na ufisadi mkubwa.
Mahakama hiyo pia imemtaka Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Brazil alipe dola laki tatu na 50 elfu kutokana na baadhi ya makosa yake
No comments:
Post a Comment