MAALIM SEIF SHARIF AKIONGEA JUU YA BODI YA MIKOPO ZNZ
NA HAMED MAZROUY
Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewataka
watendaji wakuu wa bodi ya mikopo kwa elimu ya juu Zanzibar kucha
kabisa kuwa na muhali katika utendaji wa Kazi zao.
Pia ameitaka
bodi hio kucha kuwakopesha pesa za masomo wanafunzi ambao ni watoto wa
viongozi ukizingatia wazazi wao wanauwezo wa kuwasomesha badala yake
pesa hizo wakopeshwe watoto wa maskini wasiokuwa na uwezo wakulipiwa na
wazazi wao.
Maalim Seif
amayesema hayo huko katika ofisi ya bodi ya mikopo iliopo ya zanzibar
iliopo mnazi mmoja mjini unguja kufuatia ziara yake katika taasisi
mbali mbali za secta ya elimu ziliopo Zanzibar
Na kwaupande
wake Mkurugenzi wa bodi hio ndugu Khamis Iddy amesema kuwa miongoni mwa
changamoto zinazoikabili bodi hio ni kuwepo kwa wanafunzi wengi sana
wanaomba mikopo wakati wao hawna uwezo wa kuwapatia hudunma wanafunzi
wote wanaomba mikopo kupitia bodi ya mikopo ya Zanzibar,hivo basi
ameiomba serikali kulifikiria suali hili ili kuweza kuwatatulia
changamoto zinazowakabili wanafunzi wa kizanziba.
Kufuatia
ziara hio pia alipatan nafasi ya kukitembelea chuo kikuu cha kiislamu
kilichopo chukwani nje kidogo ya mji wazanzibar na kujionea shughuli
mbali mbali ziopo chuoni hapo lakini pia amekipongeza chuo hicho kwa
kuweze kuwa na kiwanda cha uchapishaji wakati hata serikali mara
nyengine hutumia kiwanda hicho kufanya kazi zake.
No comments:
Post a Comment