Wednesday, November 28, 2012

JAPAN KUIJENGEA ZANZIBAR KIWANJA CHA MICHEZO PEMBA


Japan kuijengea Z’bar kiwanja cha michezo Pemba



Jumla ya Shilingi milioni 200 za kitanzania zinatarajiwa kutolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kugharimia Uwanja wa michezo mbalimbali utakaojengwa Kisiwani Pemba.

Hayo yameelezwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Takumi Shimojo alipokuwa akizungumza na Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk ofisini kwake leo Kikwajuni mjini Zanzíbar.
Pia amesema kuwa Serikali ya Japani inakusudia kujenga uwanja wa huo kisiwani Pemba mara tu pale nchi hiyo itakapoidhinisha kuanza kwa kazi hiyo hapo mwakani.
Amefahamisha kuwa Uwanja huo utakaojumuisha michezo ya Judo, Karatee,Mpira wa Kikapu, Tebuli tenis na michezo mingine utajengwa ikiwa ni njia ya kuimarisha mahusiano mema kati ya Japan na Zanzíbar.
Nae waziri Said Ali Mbarouk alimshukuru Balozi huyo kwa msaada wa ujenzi huo na kusema kuwa kitendo hicho ni cha kupongezwa kwa Serikali ya Japani kwani kitaiwezeshaZanzibar kutoa wanamichezo imara ambao watafadika na kiwanja hicho hususani wakaazi wa kisiwa cha Pemba.

No comments:

Post a Comment