Mfumo kristo ni nini?
Mfumo wa damu umeitwa mfumo kwa sababu damu imeenea kote mwilini.
Watu wa dini ya kikristo imehodhi asassi zote za nyeti za uongozi na
mamlaka katika nchi hii, sehemu zote za nguvu/maamuzi ya dola zimeshikwa
na wakristo tangu uongozi wa juu ikulu mpaka kiongozi wa mtaa uongozi
wote umeshikwa na mfumo kristo.
Na hao walioshika hizo nyadhifa wanazitumia kuuendeleza ukristo na
kukandamiza uislamu.
Monday, June 4, 2012
Utiaji Saini wa Mkataba wa Muungano na Matokeo Yake {UHARAMU WA MUUNGANO}
“Hapana shaka yoyote kuwa Mkataba [wa
Muungano] uliandaliwa kwa siri sana. Maofisa wawili [wa Kiingereza]
Brown na Fifoot walihusika kwa karibu sana. Hakukuwa na mshauri wa
kisheria kwa upande wa Zanzibar. Karume hakuliarifu Baraza la Mapinduzi.
Jumbe alikuwa hajui.
Inawezekana Babu alikuwa anafahamu kuwa
kulikuwa kuna kitu kinaendela, na inawezekana alishiriki katika
mazungumzo ya kijumla, lakini hakutarajia kuwa Muungano utafanyika kwa
haraka namna ile. Salim Rashid [Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi]
aliuona Mkataba [wa Muungano] kwa mara ya kwanza pale ‘bahasha yenye
Mkataba ulipowasili Ikulu kwa ajili ya kutiwa saini na Karume’.
Karume alimuelekeza Salim asimuonyeshe
Dourado ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wa wakati huo. Salim
alimuambia Karume kuwa Mkataba wa Muungano ulihitajia ushauri wa
kisheria. Salim akapanga kumleta Nabudere, wakati huo alikuwa ni
mwanasheria kijana kutoka Uganda ambaye Salim alionana naye London
lakini Nabudere alipofika Zanzibar Mkataba wa Muungano ulikuwa tayari
umo katika mchakato wa kusainiwa.
Katika mahojiano na muandishi [Issa Shivji], Nabudere alithibitisha kuwa wafuasi wa chama cha Umma, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walimuita ende Zanzibar. Alipofika Zanzibar, aliwekwa peke yake afanye kazi ndani ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Wakati huo, Mwanasheria Mkuu Dourado, alikuwa hayupo.

Nabudere alipewa kopi ya Mkataba wa
Muungano ambayo ilikuwa bado haijatiwa saini. Alitumia baadhi ya siku
kuzipitia nyaraka husika za sheria za Zanzibar na makabrasha mengineyo.
Baadae akenda Ikulu kuonana na Karume. Alimuarifu Karume kuwa kimsingi
[Muungano] ulikuwa ni uamuzi wa kisiasa. Utaifa wa Zanzibar utakabwa
sana lakini uamuzi wa mwisho wa kisiasa anao yeye Karume.
Karume akasema yeye hana matatizo na
Muungano kwa hiyo Nabudere akasema basi atakuwa hana mchango [wa
kisheria]. Baadae Karume akashuka chini na Nabudere na kumuambia kuwa
Nyerere amekuja kuonana nae. Nyerere alikuwa na Roland Brown. Jumla
walikuwepo watu wane. Nabudere akajuulishwa na Nyerere.
Hakukuwa na mazungumzo khasa juu ya
Mkataba wa Muungano. Baada ya kidogo, Nabudere akaondoka. Alipotoka nje
ya Ikulu aliwaona baadhi ya wafuasi wa Umma waliokuwa wakiupinga
Muungano. Nabudere alionana na Babu jioni ya siku ile. Inavyoonsha Babu
aliwasili Zanzibar siku hiyo hiyo.
Nabudere alimueleza Babu kuhusu mkutano
wake na Karume. Babu akasema kuwa yeye hana matatizo na Muungano.
Nabudere akasafiri asubuhi ya siku ya pili au baada ya siku moja.
Nabudere hakuweza kuzikumbuka tarehe za kuwasili na kuondoka kwake Zanzibar. Na hakushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muungano, na wala hakushiriki katika mazungumzo yoyote yale ya Mkataba wa Muungano.

Inawezekana Nabudere alifika Zanzibar
siku chache kabla ya Mkataba kutiwa saini. Inawezekana alikutana na
Karume tarehe 22 au 23 [Januari], lakini kwa vyovyote hakushiriki katika
mazungumzo juu ya Mkataba wa Muungano na wala hakutoa ushauri wowote
ule wa kisheria.
Kwa hiyo kauli alioyoitowa Dourado miaka
20 baadae kuwa Zanzibar haikupata ‘ushauri wa kisheria au wa kikatiba
kutoka kwa Mwanasheria wake Mkuu’ ni ya kweli.
Pia ni kweli kuwa Karume hakupewa
ushauri wowote ule wa kisheria, na inawezekana sana kama ilivoonekana
mara nyingi, kuwa alikuwa hajali kuhusu sheria au mambo ya kisheria
katika uendeshaji nchi au mambo mengineyo.
Jumbe aliuona Mkataba wa Muungano kwa
mara ya kwanza baada ya mawaziri wa Zanzibar kurudi kutoka Dar es Salaam
ambako walikwenda kushuhudia kuidhinishwa kwa Mkataba wa Muungano ndani
ya bunge la Tanganyika.
Jumbe anasema alimuambia Karume kuwa
kulikuwa kuna kitu hakipo barabara. ‘Vipi sisi tunayo serikali lakini
Tanganyika haina!’ Jumbe alifanya kama kusema tu. Kama ilivyo kawaida
yake, Karume akapuuza: Tutarekebisha baadae.
Kama hawana serikali [ya Tanganyika] si shauri yao wenyewe!
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini Zanzibar tarehe 22 Aprili 1964…Tamko rasmi la safari ya Nyerere kwenda Zanzibar ambayo ilikuwa ni ya mara ya kwanza kutokea kufanyika mapinduzi, ilielezewa kuwa ilikuwa ni ”safari ya heshima.” Safari hiyo ilidumu kwa masaa mawili tu.

Nyerere alikwenda na Ronald Brown na
Fiffot. Picha ya utiaji saini [Mkataba wa Muungano] ipo mpaka leo, na
inamuonyesha Abdulaziz Twala, Kasim Hanga na Ali Mwinyigogo kutoka
upande wa Zanzibar na Oscar Kambona, Job Lusinde na Bhoke Munanka kutoka
upande wa Tanganyika.”
Kuuidhinisha Mkataba wa Muungano
Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.
Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.
Mkataba wa Muungano ni mkataba wa
kimataifa ambao ulitiwa saini na viongozi wawili wa nchi mbili. Katika
mfumo wa kisheria wa kawaida ambao unafuatwa na Zanzibar na Tanganyika,
mikataba ya kitaifa inahitajia kuidhinishwa na mabaraza ya kisheria ili
kuipa nguvu za kisheria.
Kifungu viii cha Mkataba [wa Muungano]
kinasema wazi kuwa Mkataba wa Muungano ‘lazima uidhinishwe kisheria na
Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar na pamoja na Baraza la Mawaziri liidhinishe na liipe nguvu za
kisheria Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar’.
Ni muhimu kuwa kifungu hichi
hakizungumzi tu juu ya uidhinishaji wa Mkataba wa Muungano bali
kinalazimisha sharti juu ya mabaraza mawili kutoka Tanganyika na
Zanzibar kuudhinisha na kuupa nguvu kwa ajili ya serikali za nchi zote
mbili.
Hilo ndilo khasa lililofanywa na Bunge
la Tanganyika. Tarehe 25 Aprili 1964 (ambayo ilikuwa ni siku ya
Jumamosi), Rais wa Tanganyika, Julius Nyerere, aliliita bunge kwa ajili
ya kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Wajumbe wengi wa Baraza la
Mapinduzi walikuwepo wakati Bunge la Tanganyika lilipokuwa likijadili
muswada wa sheria mpya wa kuuidhinisha kisheria Mkataba wa Muungano.
Aliusisitiza uhusiano mrefu wa
kihistoria baina ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar, ambao
umeufanya muungano baina yao uwe kama ni kitu cha kawaida.
Pia alitilia nguvu hamu ya watu wa
Afrika kuujenga Umoja wa Afrika. Alilitilia mkazo suala la kuundwa kwa
shirikisho la Afrika Mashariki na kuwa Muungano baina ya Tanganyika na
Zanzibar hautoziathiri [kwa vibaya] juhudi zao katika kuelekea kwenye
Umoja wa Waafrika. Kurasa 82-83.
Wakati mchakato wa kuuidhinisha [Mkataba
wa Muungano] kwa upande wa Tanganyika ulifuatwa hatua kwa hatua na
ulifuata taratibu kama zinavatakiwa na sheria ya Mkataba wa Muungano,
hayo hayawezi kusemwa kuwa yalifuatwa kwa upande wa Zanzibar. Ukurasa
85.
Jumbe na Salim Rashid [Katibu wa kwanza
wa Baraza la Mapinduzi] wote wawili hawakubali kuwa kuliwahi kufanywa
mkutano wa Baraza la Mapinduzi kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Kwa
mujibu wa kiapo aliochoapa Salim Rashid Mahakama Kuu ya Zanzibar, katika
kesi ya Rashid Salum Adiy na watu 9 wengine dhidi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na watu 4 wengine (Nambari 20 ya
2005), ameshuhudia [Salim] kuwa hajawahi kuulizwa na wala hakuwahi
kuitisha kikao cha Baraza la Mapinduzi kuudhinisha Mkataba wa Muungano.
Hajawahi kuulizwa na hakuwahi kumpa taarifa mwandishi yoyote kuiandika
sheria ya kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Ukurasa 89.
“Katika kipindi chote cha utawala wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere, uhakika wa kisheria wa Muungano ulinyimwa jukwaa. Ikionekana ni usaliti kujadili au hata kuutaja Mkataba wa Muungano wa 1964.

Kwa vile Mwalimu Nyerere alivimiliki
vyombo rasmi vya habari na kwa sababu kulikuwa hakuna vyombo huru, maovu
yake makubwa ya uvunjaji wa Katiba hayakuweza kuripotiwa.” Profesa
Hamza M. Njozi kwenye dibaji ya kitabu cha Rais Mstaafu Mzee Aboud
Jumbe, The Partner-ship: Tanganyika Zanzibar Union 30 Turbulent years
ambacho kilichapishwa mwaka 1994 na Al Khayria Press Ltd na kuenezwa na
Amana Publishers.
Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Jumuiya ya Mataifa (United Nations)
Kutoka Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru, Ukurasa 334.
“Ukweli unabakiya kuwa Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar haukuwahi kusajiliwa katika Seketeriet ya Umoja wa Mataifa [UN].

Kwa mujibu wa Andrei Kolomoets wa Ofisii
ya Mambo ya Kisheria ya Umoja wa Mataifa “Kama ulisajiliwa basi
kungelikuwepo rekodi katika Data Base na shahada ya usajili
ingelikuwepo. Nimecheki, haipo.”
Kamisheni ya Katiba na Bunge la Katiba
Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.
Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.
Itakumbukwa kuwa Mkataba wa Muungano
uliagiza kuchaguliwa kwa kamisheni ya katiba na kufuatiliwa na bunge la
katika ndani ya mwaka mmoja kutokea siku ya kutiwa saini Mkataba wa
Muungano ili katiba ya Muungano ipatikane.
Haikufanyika na wakati wa kuyatekeleza
hayo ukaakhirishwa moja kwa moja. Kisheria ilifanywa hivyo pale bunge la
Muungano lilipopitisha Sheria ya Bunge inayoitwa Sheria ya
Bunge la Muungano, 1965 (Nambari 18)…Kwa hiyo kimyakimya, kisirisiri, bunge la Muungano limeubadilisha Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano.
Bunge la Muungano, 1965 (Nambari 18)…Kwa hiyo kimyakimya, kisirisiri, bunge la Muungano limeubadilisha Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano.
Inaweza kuhojiwa kama (a) upande mmoja
wa bunge la Muungano una mamlaka ya kuubalilisha Mkataba wa Muungano
ambao ni mkataba wa kimataifa na (b) kuibadilisha sheria ya Zanzibar
ambayo inasemekana kuwa ilipitishwa na Baraza la Mapinduzi kuudhinisha
Mkataba wa Muungano.
Inaweza ikahojiwa, na kwa njia safi na
ilio wazi zaidi, kuwa njia nzuri ingelikuwa kwa viongozi watendaji
wawili, Karume na Nyerere, na Nyerere kwa uwezo wake kama ni mkuu wa
‘Tanganyika’, angelipatana upya kuhusu Mkataba wa Muungano.
Lakini kisiasa njia hiyo ingelikuwa ni msiba kwa sababu ingeliuunja muungano hapo hapo. Ukurasa 163-164.
Kama unamjuwa adui yako na unajijuwa wewe mwenyewe, utakuwa huna wasiwasi wa matokeo ya vita hata viwe mia. Lakini kama unajijuwa wewe mwenyewe lakini humjui adui yako, basi kwa kila vita utakavyoshinda basi pia utashindwa. Na kama humjui adui yako na hujijui wewe mwenyewe basi utashindwa katika kila vita – Sun Tzu.

No comments:
Post a Comment