Shamhuna aitolea uvivu Wizara ya Elimu Tanzania
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamhuna
ameilaumu Wizara ya Elimu ya Tanzania Bara kwa kutoishirikisha Zanzibar
ipasavyo katika mabadiliko mbali mbali hususani katika suala la mitihani
ya taifa.
Ameyasema hayo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, huko makao makuu ya wizara hiyo Mazizini, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya Makamu wa Kwanza katika sekta ya elimu.
Shamhuna amesema Wizara ya Elimu Tanzania kupitia Baraza la Mitihani la Taifa, mara nyingi imekuwa ikafanya maamuzi bila ya kuishirikisha wizara ya elimu zanzibar, jambo ambalo linawapa ugumu wa kuetekeleza mipango yao ikiwa ni pamoja na kuwaandaa wanafunzi kuweza kuyafahamu mabadiliko yanayofanywa na Baraza la Mitihani na ni miongoni mwa mambo yanayowapelekea wanafunzi wa Zanzibar kutokufaulu mitihani ya taifa.
Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif amezishauri wizara hizo kukaa pamoja na kujadiliana kuhusu hatua bora za kuchukuliwa katika kuondosha tofauti hizo. Baada ya kupokea taarifa ya wizara hiyo iliyowasilishwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Abdalla Mzee, Maalim Seif alihoji uhaba wa madarasa ya kusomea pamoja na vikalio katika skuli mbali mbali Unguja na Pemba. Maalim Seif ameelezea pia haja ya kurejeshwa kwa huduma za dakhalia ili kuwaondoshea usumbufu wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali, hoja ambayo imeungwa mkono na uongozi wa wizara hiyo kwamba wamelifikiria kwa muda mrefu suala hilo licha ya kukabiliwa na ufinyu wa bajeti.

No comments:
Post a Comment