Thursday, November 29, 2012

VIETNAM YAKUBALI KUISAIDIA ZNZ KWA KILIMO


Vietnam yakubali kuisadia Zanzibar kwenye kilimo – Dk. Shein


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar. Rais Shein amewasili Zanzibar leo akitokea nchini Vetnam alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema Zanzibar itafaidika na ziara yake ya karibuni nchini Vietnam kwani nchi hiyo imepiga hatua kuwa kimaendeleo tofauti na zamani.
Rais Shein aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume, mara baada ya kuwasili akitokea kwenye ziara ya siku nne nchini Vietnam. Amefahamisha kuwa ipo haja kubwa kwa Zanzibar kuiiga Vietnam katika suala la kilimo kwani nchi hiyo imepiga hutua kubwa sana katika sekta hiyo.
Rais Shein amethibitisha kuwa Vetnam imekubali kwa muda wowote ule kuisaidia Zanziba katika kilimo. Katika ziara hiyo, Dk. Shein alikutana na Rais wa nchi hiyo, Trương Tấn Sang,  na Waziri Mkuu Nguyễn Tấn Dũng na kujadiliana na kushauriana nao mambo mbali mbali yakiwemo ya kukuza urafiki uliopo baina ya nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment