Thursday, November 15, 2012

MKUTANO WA CUF

 

NA MWANDISHI WETU; HAMED MAZROUY:

MKUTANO CUF
14-11-2012
UWANJA WA MAGIRISI TAVETA FUONI

Makamo wa kwanza wa rais ambae pia ni katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF ameitaka serikali ya mapinduzi ya zanzibar kuzisimamia sharia za nchi ili kuweza kutetea haki za wananchi.

Maalim seif ameyaeleza hayo wakati alipokua akiwahutubia wananchi na wapenzi wa cuf na wazanzibar katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa magirisi taveta fuoni zanzibar,, ambapo palihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa cuf pamoja na mawaziri wa cuf,


Aidha maalim seif amempongeza rais wa zanzibar dkt Ali mohd shein kwaa kuchaguliwa kuwa makamo mwenyekiti wa chama cha ccm hivyo amemtaka kuhakikisha vikosi vya serikali ya mapinduzi ya zanzibar vinakuepo kisheria sambamba na kufuata sheria katika utendaji wao ili kuweza kufanya kazi ipasavyo,,


Aidha maalim seif ameelezea kusikitishwa kwake na serikali kuwarejesha baadhi ya wastaaafu wa vikosi ambao walipata sifa ya kuwatesa wananchi katika kipindi cha chuki dhidi ya wazanzibar na kutakiwa kushiriki katika harakati za kutuliza fujo na ghasia zilizotokea zanzibar. hivyo amewataka wawakilishi wa zanzibar kuhakikisha wanapata majibu kutoka kwa waziri wa nchi ofisi ya rais mh Mwinyi Haji kutoa maelezo ya kurudisha wastaafu hao kwa mkataba,


Maalim seif akizungumzia muungano amesema mfumo wa muungano tulionao hivi sasa wa serikali mbili hauna faida kwa wazanzibar, hivyo wazanzibar walio wengi hawautaki na badala yake wanataka mkataba ambao utaweza kuwapa mamlaka kamili ili kuweza kujiamulia mambo wanayoyataka ili kuweza kupiga hatua za maendeleo kwa haraka. hivyo amesema njia pekee ya kuweza kujinasua katika hali hiyo ni kushiriki kwa wingi katika utowaji wa maoni ambao unategemewa kuendelea katika mkoa wa mjini maghribi kuanzia tarehe 19 mwezi huu na kuanzia katika jimbo la mtoni,


Katika mkutano huo maaalim Seif ameweza kuwakabidhi kadi wanachama wapya 92.

No comments:

Post a Comment