NASAHA KWA WAISLAM WOTE
ASSALAM ALAIKUM WARAHMATULLAHI WABARAKATUH
NA Omar Abdalla Alpembawiy
WANAKHALIFU AMRI YA ALLAH NA MTUME WAKE KWA SEHEMU NDOGO YA DUNIA.
Ndugu zangu waislamu hasa tunaoishi zanzibar lini tutamuogopa Allah
na kufuata amri alizokuja nazo mtume saw?Viongozi waislamu wamesahau
wao wameumbwa kwa makusudio gani na hii dunia ni sehemu ya mapito,vyeo
vyao leo na kesho havipo baada ya kuitwa Muheshimiwa ataitwa Maiti ama
Marehemu unajitangulizia nini mbele ya Allah swt. Ikiwa wewe una kuwa
mkali watu kuvunja sheria mulizo zipanga kwa mikono yenu jee zile za
muumba wa mbingu na ardhi na vilivyo ndani yao munazivunja tena kwa
kibri na kujifakhiri? Allaha anasema
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا
قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ
أَمْرِهِمْ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا
مُبِينًا
(36 Haiwi kwa Muumini mwanamume wala mwanamke anapohukumu
jambo Allah na mtume wake kuwa na khiyari juu ya mambo hayo
yaliyohukumiwa.na yeyote atakaye muasi Allah na mtume wake wamepotea
upotevu ulio mkubwa.
Ndugu zangu viongozi huwa wakali sana
kuvunjwa sheria walizopanga huku wakisahau wao ni wavunjifu wakubwa wa
sheria za Allah na mtume wake vipi utatiiwa wakati wewe mwenyewe ni
muasi? Mtume ametukataza kutii viongozi waasi wanaovunja amri za allah
na Mtume wake kama alivyotuambia katika hadithi yake tukufu.
عَنْ
جَدِّهِ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى الله
عَليْهِ وسَلَّمَ قَالَ : سَيَلِي أُمُورَكُمْ بَعْدِي ، رِجَالٌ
يُطْفِئُونَ السُّنَّةَ ، وَيَعْمَلُونَ بِالْبِدْعَةِ ، وَيُؤَخِّرُونَ
الصَّلاَةَ عَنْ مَوَاقِيتِهَا فَقُلْتُ : يَا رَسُولَ اللهِ ، إِنْ
أَدْرَكْتُهُمْ ، كَيْفَ أَفْعَلُ ؟ قَالَ : تَسْأَلُنِي يَا ابْنَ أُمِّ
عَبْدٍ كَيْفَ تَفْعَلُ ؟ لاَ طَاعَةَ ، لِمَنْ عَصَى اللَّهَ.
Hakika ya mtme saw alisema yatafuatia mambo baada yangu,kuna watu watafanya
bidii kufuta suna zangu(mienendo)na watafanya mambo ya uzushi(watazua
yao)na watachelewesha swala kutokana na wakati wake,swahaba akasema
ikiwa hivyo tufanye vipi?mtume akamwambia unaniuliza mimi?musitiie
yeyote anayemuasi allah.
Hivyo ndugu zangu kitendo cha kiongozi
kutaka kutiiwa sharti naye awe anamtii allah na mtume wake si hivyo
utakuwiyeni wakati mgumu na kitakachokufuatia ni kudhulumu na kuadhibu
munaowaongoza kwa kuwapiga,kuwauwa na kuwatia jela.kwani kumbuka
unayemuongoza ni binadamu mwenye akili timamu anajuwa zuri na baya.hivyo
mtu hawezi kutii ikiwa wewe ni asi mkubwa wa Amri ya Allah na Mtume
wake na kuzidisha ushahidi wa hilo mtume amesema
عَنْ عَلِيٍّ ،
رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم بَعَثَ
جَيْشًا وَأَمَّرَ عَلَيْهِمْ رَجُلاً فَأَوْقَدَ نَارًا وَقَالَ
ادْخُلُوهَا فَأَرَادُوا أَنْ يَدْخُلُوهَا وَقَالَ آخَرُونَ إِنَّمَا
فَرَرْنَا مِنْهَا فَذَكَرُوا لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ
لِلَّذِينَ أَرَادُوا أَنْ يَدْخُلُوهَا لَوْ دَخَلُوهَا لَمْ يَزَالُوا
فِيهَا إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَقَالَ لِلآخَرِينَ لاَ طَاعَةَ فِي
مَعْصِيَةٍ إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ.
Sayyidina
Ali r.a ziwe juu yake amesema kuwa Mume alituma jeshi kwenda jihadi
akamfanya mmoja wao kuwa Kiongozi wao.yule kiongozi akawasha moto na
akawataka wale anaowaongoza wengine ndani ya moto ule.kundi moja
likataka kuingia moja likasema sisi tumeukimbia huo itakuwaje tuingie
ndani ya moto huo? Akazungumziwa mtume juu ya jambo hilo akawambia wale
waliotaka kuingia laiti mungaliingia basi mungelikaa humo mpaka siku ya
kiyama .na akawambia wale wengine hakuna kutii katika jambo la maasi
hakika ya kutii ni kwa mambo mema.
Tunajifundisha nini?hatuwezi
kutii viongozi ambao wao wenye ni waasi wa Amri za Allah na Mtume wake
tena kwa viburi na kujifakhiri,ndani ya Zanzibar yetu wamechukuiliwa
mashekhe kwa tuhuma ya kuwa wamevunja sheria na wamewekwa ndani kwamba
uchunguzi unafuatiliwa. Oky ni sawa kabisa jee hawa waliovunja sheria ya
binadamu tena hakuna uhakika kwa kuwabambikia kesi za uongo lengo kuwa
dhulumu tu na wale wanaovunja Amri za Allah na Mtume wake wabaya na
wakosa zaidi ni nani?Viongozi hawa hawa baada ya kuwatia ndani mashekhe
hao ni mahabusu na watuhumiwa hawajahukumiwa wanawachukuwa na kuwanyowa
ndevu zao jambo ambalo ni makosa makubwa jee hawa kweli wanafuata sheria
au wanafuata matamanio ya nafsi zao. Mtume saw amesema:
عَنِ
ابْنِ عُمَرَ ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : خَالِفُوا
الْمُشْرِكِينَ وَفِّرُوا اللِّحَى وَأَحْفُوا الشَّوَارِبَ
hadithi inatokana na Ibin Umar anasema kuwa mtume saw alisema
wahalifuni washirikina (mayahudi,manaswara.na wamajusi)na fugeni ndevu na nyoeni masharubu.
Hivi leo inakuwaje kuwatii watu amabao wanamuasi Allah na mtume na
wanafuata mayahudi na manaswara?wanapinga suna ya mtume swa ambaye
hatamki kwa matamanio yake lengo tu kufurahisha mabwana zao wa dunia
mayahudi na manaswara.uislamu umeharamisha kabisa sisi kujifananisha na
mayahudi na manaswara kivyovyote vile au wamajusi lakini leo ndiyo
shabaha ya viongozi hao amabao wanagomba kuvunjwa sheria zao wakati wao
moja kwa moja wanzipinga amri za muumba mtume amesema
إن أهل الشرك يعفون شواربهم ويحفون لحاهم
فخالفوهم فاعفوا اللحى وأحفوا الشوارب.
Hakika Mayahudi na Manaswara na Mamajusi hufuga masharubu yao na
hunyoa ndevu zao wakhalifuni musiwafuate,nyinyi fugeni ndevu zenu na
nyoeni mashurubu yenu.
Huu ni mtihani mkubwa yaani waislamu
wanavunja amri za Allah na mtume wake huku wakijisifu UAMSHO kwisha Inna
lilah wa inna ilayih Raajiuun,tena kuna na gwaride linachezwa
tumewanyoa ndevu zao tumewaungusha.wewe ni muislamu lini utamtii mola
wako ?lini utamtii mtume wako?unafurahi kuwaaasi kwa kufurahisha mabosi
wako? Juwa siku ya kiyama kila mtu atabeba mzigo wake na hao
waliokuamrisha kufanya hivyo watakuruka mbele ya Allah.tuko tayari kuwa
fuata ahli shirki huku tukifurahi kumuasi allah na mtume wake? Maana
vitendo vya kunyoa ndevu na kuacha masharubu ni mila yao siyo ya
kiislamu mtume anasema
( إن فطرة الإسلام الغسل يوم الجمعة
والاستنان وأخذ الشارب وإعفاء اللحى فإن المجوس تعفي شواربها وتحفي لحاها
فخالفوهم حد'وا شواربكم واعفوا لحاكم )
Hakika katika
mienendo ya uislamu au maumbile ni kuoga siku ya Ijumaa kujisuwaki,na
kunyoa masharubu na kuziwacha ndevu kwani hakika ya Wamajusi hufuga
masharubu yao na kunyoa ndevu zao basi wakhalifuni nyoeni sharubu fugeni
ndevu.
Tujiulizeni wale waliofanya vitendo haramu vya kunyoa
ndevu waislamu watuhumiwa na wale waliofurahia juu ya jambo hilo
watakwenda kumeleza nini Allah siku ya kiyama siku amabayo atatupa kila
anayenyonyesha kila anachonyonyesha ,na kuzaa kila kilicho bebwa katika
matumbo hata kama ni wiki mbili kwa mshituko wa siku hiyo halafu
tutajiuliza kwanini sisi siku zote nchi zetu zinakuwa maskini jawabu ni
kumuasi allah na viongozi waovu na Allah anasema فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ
يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَنْ تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ
عَذَابٌ أَلِيمٌ (63
Basi nawahadhari wale ambao huhalifu amari zake(Allah na Mtume wake)kuwamiminikia fitina ama adhabu iumizayo.
Ndugu zangu tujitahidi kumtii allah ana kuyasema dhulma
zinazofanywa kadri ya uwezo wa mtu alivyojaaliwa ili tusije tukapambana
na adhabu hiyo.tujirekebisheni na viongozi wajirekebishe kwani kufanya
hivyo wanavyofanya ni kufuata mayahudi mna manasara na tumeambiwa « مَنْ
تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ ».mwenye kujifananisha na wtu fulani
naye ni miongoni mwao.hayo ni maneno ya mtume maana siku zote ukisema
ukweli unaambiwa unatukana.kwa kuongezea mtume amesema ليس منا من تشبه
بغيرنا لا تشبهوا باليهود ولا بالنصاري si katika sisi anayejifananisha na
wasiokuwa sisi,musijifananishe na mayahudi na manaswara.sasa tujiulize
kunyowa watu ndevu ni kujifananisha na akina nani?Allah tuongoze
inshallah
ALLAH ATUWAFIKISHE INSHALLAH
No comments:
Post a Comment