Sunday, December 30, 2012

AJALI MBAYA YA GARI WILAYA YA KASKAZINI A UNGUJA

29 2012

 
 
 
 
 
 
Rate This

PICHA HII SIO HALISI
PICHA HII SIO HALISI

Wafanyakazi wa Drime Hotel ilopo Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini wilaya ya kaskazini A Unguja jana majira ya saa 12 joni wamepata ajali huko maeneo ya kilima cha Mchakaeni kilichopo Pwani mchangani baada ya Dereva wa gari hio kuzidiwa nguvu kutokana na mwendo mkubwa uliokuwa ikitembea gari hio
Idadi ya wafanyakazi waliokuwemo ndani ya gari hio ni watu wasiopunguwa 26,jumla ya majeruhi ni kumi tano kati yao watatu hali zao sio za kuridhisha lakini wote mpaka sasa wameshafikishwa katika hospitali ya Alrahma iliopo kilimani wilaya ya mjini unguja kwa ajili ya matibabu zaidi,
Mara tu baada ya kutokea kwa ajali hio aliekuwa dereva alie juulikana kwa jina la Said Omar  alitoweka na kukimbia ghafla kwenye eneo la tukio, kwa mujibu wa taarifa zimesema kuwa  dereva huyo ndio mara yake ya mwanzo kufaya kazi katika Hoteli hio.
Kufuatia tokeo hilo mwandishi alifanikiwa kuongea na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Nd,Mussa Ali Mussa kwa lengo lakupata taarifa zaidi kuhusiana na ajali hio lakini kamishna huyo alisema hana taarifa mpaka sasa ila aliamuru tumtafute kamada wa Polisi wa mkoa wa kaskazini Unguja  lakini jitihada zilishindwa kufanikiwa kutokana na tatizo la mawasiliano.

No comments:

Post a Comment