Desemba 17, 2012
Al-Shabaab ilitangaza siku ya Jumatatu (tarehe 17 Disemba) kuwa
imevunja uhusiano wake na mwanajihadi mzaliwa wa Marekani Omar Hammami,
maarufu kama Abu mansoor al-Amriki.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, al-Shabaab ilimshutumu Hammami, mwenye umri wa miaka 28, juu ya majivuno na mlipizaji kisasi katika kutoa video na taarifa za madai kuwa alikuwa anatishiwa na wapiganaji wenzake na kwamba al-Shabaab inakabiliwa na mizozo ya ndani.
“Kutokana na matukio haya, na kwa ajili ya ufafanuzi juu ya utatanishi unaohusu suala la Abu Mansoor, Harakat al-Shabaab al-Mujahideen hapa tunathibitisha kuwa Abu Mansoor kwa njia yoyote ile, ya umbo au mtindo, hawakilishi maoni ya mujahidina wa Somalia,” taarifa ya al-Shabaab ilisema.
Hammami huko mwanzo alionekana kama kiongozi muhimu wa kigeni ndani ya al-Shabaab, na mwezi uliopita aliwekwa kwenye orodha ya Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI) kama gaidi anayetafutwa sana.
Ikiripotiwa kuwa yuko nchini Somalia tangu mwaka 2006, alito video hapo kabla zinazotoa wito kwa uandikishaji wa askari wa kigeni, ikiwa ni pamoja na kuimba nyimbo za rap kwa lugha ya Kiarabu za kusifia jihadi, licha ya ukweli kwamba al-Shabaab wanapiga marufuku mziki katika tafsiri yake kali juu ya Uislamu.
Al-Shabaab bado wanatafuta kuandikisha wageni, taarifa hiyo ilisema. "Jukwaa la jihadi hata hivyo linapokea watu wa aina zote. Wengine, juu ya wengine, mara kwa mara huinuka kwa umaarufu na mara nyingi kuwa na faida ndogo isipokuwa kwa upekee wao," taarifa ilisema.
Huko nyuma Hammami alionekana kuwa kiongozi wa wapiganaji wa kigeni ndani ya al-Shabaab, sambamba na makamanda wa juu wa Somalia kama Sheikh Mukhtar Robow Ali, known as Abu Mansur, na Sheikh Hassan Dahir Aweys, ambaye hivi sasa al-Shabaab inajaribu kumuua.

No comments:
Post a Comment