Tuesday, December 18, 2012

2 wajeruhiwa katika mlipuko wa Eastleigh, 9 watiwa mbaroni


Desemba 17, 2012


Watu wawili walijeruhiwa vibaya sana siku ya Jumapili (tarehe 16 Disemba) wakati kiasi cha maguruneti matatu yalipotupwa katika baa kwenye kitongoji cha Eastleigh cha Nairobi, AFP iliripoti.
"Wale walioyarusha (maguruneti) wanawezekana walikuwa wamepiga kambi katika jengo la jirani, lakini tunawashikilia washutumiwa tisa kwa mahojiano," Afisa wa Polisi Mkoa wa Nairobi Moses Ombati aliiambia Sabahi.
Polisi wamewatia mbaroni Wayemeni wanane na Msomali mmoja kuhusiana na shambulio la Jumapili, alisema. Ombati alisema kuwa watu wenye utaifa wa Yemen walikuwa wamepanga nyumba karibu na eneo la mlipuko na yule mwenye uraia wa Somalia anasemekana ni mshughulikiaji wa nyumba hiyo. Alisema kuwa wataisaidia polisi katika uchunguzi.
Tukio hilo lilitokea karibu na msikiti wa Hidaya, ambao ulilengwa katika shambulio la tarehe 7 Disemba ambalo liliua watu sita na kumjeruhi mbunge wa eneo hilo Yusuf Hassan.
Ombati alisema kuwa polisi watazidisha doria na misako ya magaidi na kuzuwia mashambulizi zaidi.

No comments:

Post a Comment