Desemba 24, 2012
Jaji Mkuu Willy Mutunga alimwapisha David Kimaiyo kuwa inspekta mkuu
wa kwanza wa polisi wa Kenya hapo Jumatatu (tarehe 24 Disemba), Capital
FM ya Kenya iliripoti.
Akiwa afisa wa polisi, Kimaiyo alihudumu kama kamanda wa kikosi cha msafara wa rais, kamanda wa Kitengo Maalum cha Polisi, mkurugenzi wa operesheni kwenye Makao Makuu ya Polisi ya Kenya na mkurugenzi wa Kikosi cha Taifa kinachohusika na Silaha Ndogo Ndogo.
Changamoto kadhaa zinamsubiri Kimaiyo wakati anapochukua nafasi hii mpya, ikiwemo harakati za kigaidi zinazohusishwa na al-Shabaab, kurudi kwa ghasia kwenye eneo la Tana River Delta na uchaguzi mkuu wa mwezi Machi 2013.
"Nawahakikishia Wakenya wote kwamba Jeshi la Polisi la Kenya litamshughulikia ipasavyo mtu yeyote yule atakayejaribu kuhujumu uchaguzi wa amani nchini Kenya," alisema. "Hatutavumilia matendo yoyote ya ghasia wakati wa kipindi hiki muhimu."
Kimaiyo pia aliahidi kushirikiana na Kamisheni ya Jeshi la Polisi na Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi kutenga fedha na vifaa vya kutosha kwa maafisa wa polisi.
"Mfumo wa sasa wa malipo ni wa zamani sana, haukutengenezwa kukabiliana na mabadiliko makubwa kwenye majukumu ya polisi kwa miaka kadhaa sasa," alisema Kimaiyo.

No comments:
Post a Comment