Desemba 24, 20
Kikosi cha Polisi wa Majini wa Puntland hapo Jumapili (tarehe 23
Disemba) kiliwaokoa mabaharia 22 wa meli ya MV Iceberg 1, ambao walikuwa
wametekwa na maharamia wa Kisomali kwenye pwani ya Gara’ad kwa takriban
miaka mitatu.
Polisi waliwaokoa mateka hao baada ya maharamia kutoroka kutoka meli hiyo, naibu mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Puntland, Jenerali Muhiyadin Ahmed Muse, aliiambia Sabahi. Kikosi Polisi wa Majini cha Puntland kilianza juhudi za kuwaokoa mateka hao mnamo tarehe 10 Disemba.
“Mateka hao walikuwa na alama za mateso na utapiamlo na sasa wako kwenye mikono ya vyombo vya usalama,” alisema Muse. “Tunafanya kazi ya kuwatibu na kuwalisha. Wamerufahi baada ya kuwapangia kuzungumza na familia zao.”
“Puntland imedhamiria kutokaa kimya wakati maharamia wanafanya matendo kama hayo, na tunakusudia kuwang’oa kupitia operesheni inayofanywa kwenye fukwe na miji,” alisema Muse.
Meli ya MV Iceberg 1 inayomilikiwa na Dubai na yenye bendera ya Panama ilitekwa mwezi Machi 2010, ikiwa na mabaharia 24 kutoka Ghana, India, Pakistan, Ufilipino, Sudan na Yemen.
Mamlaka za mkoa wa Puntland hazikutoa ishara yoyote ya majaaliwa ya mabaharia wawili waliopotea au ikiwa maharamia bado wako hai kufuatia operesheni hiyo ya uokozi, liliripoti shirika la habari la AFP.
Baada ya kuanza operesheni wiki zilizopita, polisi waliweza kuizunguka meli hiyo na kuwakatia huduma maharamia hao, kuwanyima chakula na maji, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka utawala wa mkoa wa Puntland.
Wakaazi wa Gara’ad walisema walishajaribu mara kwa muda mrefu kuwashawishi maharamia kuwaachia mateka hao.
“Mara moja waliwaleta wengi wao ufukweni, lakini maharamia wakakataa kuwaachia hadi meli hiyo ilipokwama na kuanza kuota kutu kwenye ufukwe,” alisema Mohamed Siyad Dahir, 42. “Tulifurahi walipoachiliwa leo kwa sababu walikuwa watu wasiokuwa na hatia waliokamatwa visivyo haki.”

No comments:
Post a Comment