Tuesday, December 18, 2012

Kiongozi wa al-Shabaab akiri kushindwa

Na Majid Ahmed, Mogadishu

Desemba 17, 2012
Kiongozi wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane amekiri hadharani kuwa wapiganaji wa kikundi hiki wameshindwa katika mfululizo wa mapigano ya hivi karibuni nchini Somalia.
  • Wanachama wa al-Shabaab wasalimu amri kwa vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia huko Garsale, kilometa 10 kutoka Jowhar, tarehe 22 Septemba. [Mohamed Abdiwahab/AFP] Wanachama wa al-Shabaab wasalimu amri kwa vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia huko Garsale, kilometa 10 kutoka Jowhar, tarehe 22 Septemba. [Mohamed Abdiwahab/AFP]
  • Askari wa Jeshi la Taifa la Somalia wakifanya doria Jowhar tarehe 10 Disemba baada ya kunyang'anya mji huo kutoka kwa al-Shabaab. Kupoteza Jowhar kunachukuliwa kama kipigo kikubwa kwa kikundi hiki cha wanamgambo. [Stuart Price/AU-UN IST/AFP] Askari wa Jeshi la Taifa la Somalia wakifanya doria Jowhar tarehe 10 Disemba baada ya kunyang'anya mji huo kutoka kwa al-Shabaab. Kupoteza Jowhar kunachukuliwa kama kipigo kikubwa kwa kikundi hiki cha wanamgambo. [Stuart Price/AU-UN IST/AFP]
"Mwaka huu umekuwa wa vita vitakatifu dhidi ya utawala wa Kiislamu nchini Somalia ambavyo vimekuwa vikiongezeka na adui wa vita hivi vitakatifu ameongeza jeshi lake, usalama, uwezo wa kisiasa na wa vyombo vya habari kufifisha mwanga wa sharia na kuushinda utawala wa Kiislamu," alisema katika ujumbe wa sauti wa kwenye redio uliotolewa Jumanne (tarehe 11 Disemba) na mfuko wa al-Kataib, kituo cha habari cha al-Shabaab, na tovuti nyingine zilizo shirika na kikundi hiki.
Godane, ambaye pia anajulikana kama Mukhtar Abu al-Zubair, alitangaza kuwa al-Shabaab itategemea mbinu za vita vya msituni. "Ningependa kuwaambia taifa la Kiislamu na Wajahideni wake wasomi, hususani Mullah Omar na Shekhe Ayman al-Zawahiri […] kuwa jeshi hilo linaweza kuwa la Kijahidini nchini Somalia na kwamba wametikisa jihadi ya kiroho ambayo inategemea kushambulia na mapigano kuleta hali isiyo na utulivu kwa adui katika maeneo anayoyadhibiti," alisema.
Ujumbe wa Godane ulikuja siku mbili kabla ya wapiganaji wake kukimbia mji wa Jowhar, mji mkubwa kabisa uliokuwa umebakia chini ya udhibiti wao, wakati Askari kutoka Jeshi la Taifa la Somalia na Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia walipokuwa wanaukaribia. Jowhar, mji mkuu wa mkoa wa Shabelle ya Kati, ni mmoja wa miji mikuu ya kanda uliotekwa na vikosi washirika wa serikali mwaka jana, ikiwa ni pamoja na Kismayu, Marka, Beledweyne, Baidoa na Hudur.
Kanali mstaafu Omar Mohamed, mshauri wa jeshi la Somalia, alisema tangazo la Godane kwamba kundi lake linaelekea katika vita vya msituni na mbinu za mashambulio ya kuvizia linaonyesha kuongezeka kwa udhaifu wa al-Shabaab.
"Ujumbe wa Godane unaonyesha kushindwa kabisa kutokana na kikundi kinavyopata mateso, pamoja na hali ya kukata tamaa ambayo inawahuzunisha wanachama wake wahalifu," aliiambia Sabahi. "Anachojaribu kufanya ni kuongeza hamasa ya wapiganaji wake waliokata tamaa."
"Kama tukiangalia muda wa ujumbe huu, unakuja wakati al-Shabaab iko katika kuzingirwa pande zote na inakumbana na upotezaji mkubwa siku hadi siku kutokana na mapigo makubwa ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo kutoka kwa jeshi la taifa na washirika wake," alisema. "Wanachama wa wapiganaji wa al-Shabaab wanaishi katika hali ya kukata tamaa na udhaifu kwa kuwa hawawezi kukwepa kubanwa kwa nguvu na vikosi vya jeshi vya taifa."
Mohamed alisema wapiganaji wa al-Shabaab hawana uchaguzi mwingine wowote bali kuweka chini silaha zao na kujisalimisha kwa serikali. "Wanakimbia katika miji mikubwa na kupata hifadhi katika maeneo ya vijijini ambayo yako mbali sana na vikosi vya washirika, lakini hawawezi kupata mahali salama pa raha popote pale nchini."

Rais Mohamud atangaza kushindwa kwa al-Shabaab

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud wiki iliyopita alisema kwamba al-Shabaab wameshindwa kijeshi.
"Tumelazimisha kushindwa kwa jeshi katika al-Shabaab na jeshi la taifa limekomboa miji mikubwa ya Somalia iliyo mingi," aliliambia Shirika la Utangazaji la BBC Somali tarehe 12 Disemba.
Rais alisema kwamba serikali iko tayari kuwasamehe wapiganaji Wasomali, hasa vijana, ambao wako tayari kuachana na vurugu na kuweka silaha zao chini ili kusaidia kuijenga nchi upya. "Tunawakaribisha kwa mikono miwili wasichana na wavulana wote ambao waliamua kuachana na al-Shabaab; hawa ni wasichana na wavulana wetu," alisema.
"Tunafanyia kazi kuwapeleka viongozi wa wazee kuwashawishi vijana ambao wamedanganywa kujiunga na al-Shabaab, kuacha vurugu na kuweka chini silaha zao," aliongeza.
Mohamud alisema serikali ya Somalia haitaweza kufanya mazungumzo na wapiganaji wa kigeni, kwani ni lazima warejee katika nchi zao. "Kuna fursa pia ya mazungumzo na watu ambao wanadhani wanaweza kutimiza lolote kwa kutumia silaha au kuunga mkono mauaji ya halaiki wa Somalia," alisema.
Abdirahim Issa Adow, mkurugenzi wa Redio Mogadishu na msemaji wa zamani wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu, alisema hali ya al-Shabaab kama kundi la kijeshi linakaribia limekwisha.
"Kama miaka miwili iliyopita, al-Shabaab lilikuwa ni kundi ambalo lilisaidia jeshi kwani lilizindua kampeni iliyoitwa 'Mwisho wa Wachokozi' na kutoa wito kwa vikosi vya kijeshi vya serikali na viongozi wa ngazi za juu kunyoosha mikono ndani ya siku tano," aliiambia Sabahi. "Lakini sasa, al-Shabaab wamefikia mwisho na hakuna lolote zaidi ya mabaki yaliyotegwa katika maeneo machache."
Katika ujumbe wa Godane, aliwasifia wapiganaji wa jihadi huko Afrika ya Kaskazini na Rasi ya Arabia. Adow alisema marejeo haya ni majaribio ya kuchepusha umakini dhidi ya uharibifu wa kundi. "Pia ni uangalizi wa kukatisha tamaa dhidi ya ushirikiano na uhusiano na vikundi vingine vya magaidi katika kanda," alisema.
Omar Dahir, mchambuzi wa masuala ya usalama na mkurugenzi wa kituo cha Usawazishaji na Mazungumzo huko Mogadishu, ulieleza ujumbe wa Godane ulioonyesha kuongezeka kushindwa kwa al-Shabaab kijeshi na kisiasa.
"Kwa sababu ya njia yake yenye msimamo mkali, kufuatwa kwa jihadi ya ulimwengu na muungano wake na al-Qaeda, al-Shabaab imepoteza upiganaji halisi, ambao ni kuishawishi mioyo na mawazo ya watu wa Somalia," aliiambia Sabahi.

No comments:

Post a Comment