Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ametuma
salamu za pongezi kwa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa
kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe
la challenge.
Zanzibar Heroes imeingia hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Burundi
kwa mikwaju ya penalti (6-5) kwenye uwanja wa Lugogo mjini Kampala,
Uganda kufuatia timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika dakika
zote 90 za mchezo.
Katika salamu hizo Maalim Seif alisema Zanzibar Heroes wanaendelea
kudhihirisha uwezo wa Zanizbar wa kuweza kushiriki katika mashindano ya
kimataifa.
Ameitaka timu ya Zanzibar Heroes kuongeza juhudi katika mchezo wake
wa nusu fainali ili kuendeleza ushindi wake na hatimaye kuweza kutwaa
Kombe hilo la Challenge katika msimu huu.
Na Hassan Hamad OMKR.
No comments:
Post a Comment