Wednesday, December 19, 2012

MATOKEO YOTE YA MAONI JUU YA KATIBA MPYA KWA ZANZIBAR NZIMA HAYA HAPA




MWANANCHI AKITOA MAONI YAKE JUU YA KATIBA MPYA  
MWANANCHI AKITOA MAONI YAKE JUU YA KATIBA MPYA
 
Tume ya kukushanya maoni juu ya katiba mpya imemaliza leo rasmi kazi yake hio huku takribani ya wakaazi waliowengi sana wamepata kutoa maoni yao kama hivi ifuatavo. Ukichukua mwelekeo wa maoni yote yaliyotolewa hadharani katika mikutano yote iliyofanywa na Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba katika visiwa vya Zanzibar unapata picha ifuatayo:
Waliotaka Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kufuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanga
nyika ni 14,998 sawa na 65.98%.
Waliotaka muundo wa sasa wa Muungano (Serikali Mbili) uendelee ni 7,034 sawa na asilimia 30.94%.
Waliotaka Serikali Tatu ni 105 sawa na 0.46%.
Waliotaka Serikali Moja ni 22 sawa na 0.9%.
Waliotoa maoni mengine ni 573 sawa na 2.52%.
MTAZAMO BINAFSI: Inafurahisha kuona wapenda mabadiliko (progressives) katika Zanzibar kwa ujumla asilimia yao imebakia takriban ile ile 66% ambayo ndiyo iliunga mkono kuanzishwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2010. Kwa upande mwengine, wahafidhina wanaokataa mabadiliko katika jamii ya Zanzibar wanazidi kupungua kutoka asilimia 33% hadi asilimia 31%

No comments:

Post a Comment