Dec
30
2012
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu Mstaafu wa Hesabu za Serikali wa Serikali ya Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Bwana Mohd Aboud Mohd aliyefariki Dunia Nchini
India amezikwa katika makaburi ya Wangazija yaliyopo Kisutu Mjini Dar
es salaam.
Mamia
ya waislamu, familia, wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania walihudhuria
mazishi hayo wakati wa jioni.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu
wake Dr. Mohd Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,
Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere Dr. Salim Ahmed Salim na Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa SMT walikuwa miongoni mwa watu
waliohudhuria mazishi hayo.
Marehemu
Mohd Aboud Mohd maarufu Mfaransa alizaliwa Zanzibar Tarehe 25/1/1927
na kupata elimu zake za Dini na Dunia na alipomaliza masomo yake ya
sekondari aliajiriwa serikalini mnamo tarehe 1/1/1944.
Marehemu
Mohd Mfaransa kwa umahiri wake wa utumishi serikalini alipata fursa ya
kupandishwa daraja hadi kufikia kuwa msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1967.
Rais
wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume alimpendekeza Mzee Mohd
Mfaransa kushika wadhifa wa Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 1/3/1967.
Tarehe
16/10/1967 Marehemu Mohd Mfaransa aliteuliwa rasmi Mtanzania na
Mwafika wa kwanza baada ya Uhuru wa kuwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu
za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wadhifa aliokuwa nao
hadi kustaafu kwake tarehe 25/12/1987.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Matehemu mzee Mohd Aoud Mohd {Mfaransa } mahala pema peponi amin.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziba
No comments:
Post a Comment