Press Release:-
.
Uzinduzi
huo utakaoshirikisha wananachi wa Mkoa wa Dar es salaam na Vitongoji
vyake wakiwemo pia waalikwa kutoka sehemu mbali mbali za mikoa ya
Tanzania utafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Wajumbe
wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2012
walikutana pamoja na mambo mengine katika kikao chao cha 10 walipitia
ratiba ya shughuli hiyo kwa matayarisho ya mwisho chini ya Mwenyekiti
mwenza wa Kamati hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mjini Dar es salaam.
Akiwasilisha
Taarifa za kazi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la Sensa kwa wajumbe
wa Kamati hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
Dr. Albina Chua alisema kazi ya miongozo ya Takwimu hivi sasa inaendelea
vyema.
Dr.
Albina Chua alifahamisha kwamba miongozo hiyo inakwenda sambamba na
kuhakiki taarifa na kuanza kwa zoezi la uingizaji Taarifa katika
compyuta kazi inayofanywa na wataalamu wa Takwimu baada ya kupata
mafunzo maalum ya wiki sita.
“
Jumla ya watu mia nne walilazimika kuwajiriwa kufanya kazi hiyo muhimu
inayohitaji utaalamu na umakini wa hali ya juu katika kuikamilisha
hasa kwenye uchambuzi wa takwimu za Sensa “. Alifafanua Dr. Albina Chua.
Naye
Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.
William Mgimwa alisema Wizara ya Fedha itaendelea na uchambuzi wa
Takwimu zitakazotokana na sensa hiyo kwa lengo zaidi la kiuchumi.
Dr.
Mgimwa alisema katika kukamilisha zoezi zima la sensa ya watu na makazi
Serikali imeshatoa shilingi Bilioni sita kati ya Bilioni 12
zilizotengwa ambapo kazi ya usafirishaji vifaa vya sensa imeshafanywa na
hivi sasa uingizwaji wa taarifa katika Kompyuta unaofanywa na Wahariri
maalum inaendelea.
“
Tumefanikiwa vyema katika kazi hii muhimu licha ya changamoto ndogo
ndogo zilizojichomoza katika zoezi hili ikiwemo madai ya Wenyeviti wa
Vijiji waliosaidia kusimamia zoezi hili katika maeneo yao”. Alifafanua
Waziri Mgimwa.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Zanzibar Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini kwa niaba ya Waziri
anayesimamia Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar alisema
zoezi la sensa kwa kiasi kikubwa limefanikiwa vyema licha ya changamoto
za baadhi ya vikundi vya kidini kupinga Zoezi hilo.
Dr.
Mwinyihaji alieleza kwamba sensa ya watu ambayo inakusanya takwimu
tofauti itasaidia chachu ya maendeleo hasa katika mpango wa maendeleo
katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Akitoa
nasaha zake Mwenyekiti mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya watu
na makazi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
amewapongeza watendaji wa sekta tofauti Nchini waliojitolea kufanikisha
zoezi zima la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Balozi
Seif alisema zoezi hilo lilikumbwa na changamoto zilizopelekea
kuongezwa kwa siku za uandikishaji kutokana na sababu za baadhi ya
makundi ya dini kushawishi wananchi kutojiandikisha kwenye zoezi hilo.
Kikao
cha kumi na moja cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi
kinatarajiwa kufanyika Zanzibar mnamo Wiki ya Pili ya Mwezi wa Machi
mwaka 2013.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzi
No comments:
Post a Comment