Wednesday, December 26, 2012

Padri ajeruhiwa kwa risasi Zanzibar

Father Ambros Mkendwa aliejeruhiwa kwa kupigwa Risasi na watu wasiojuulikana

 
 
 
 
 
 
Rate This

Padri mmoja mwenye kujulikana kwa jina la Amros Kwendwa wa Kanisa la Wasabato Tomondo apigwa risasi  na watu wasiojuulikana katika maeneo ya mkunazini akiwa kwenye safari ya kuelekea nyumbani kwake.
Padri huyo anawaongoza waumini wa Dini ya kikiristo katika kanisa la wasabato Tomondo hadi muda huu bado haijajulikana ni nani walihusika na tokeo hilo lililomsababishia majeraha Padri huyu zaidi maeneo ya kichwani.
Na kwaupande wake Askofu wa Anglikan Michael Hafidh amesema bado kwa sasa ni mapema mno kuelezea kama majeruhi huyo ataendelea kuwepo hospitalini hapo au atasafirishwa kupelekwa sehemu nyengine kwa ajili ya matibabu zaidi lakini pia amelaani  kitendo cha kuhujumiwa kwa viongozi wa dini.
Kwa upande wa jeshi la polisi umethibitisha kutokea kwa tokeo hilo huku wakisema kuwa hakuna mtu yoyoyte alishikiliwa hadi sasa lakini limesisitiza bado linaendelea na uchunguzi na atakaebainika basi atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment