Polisi yakamata viongozi wengine wa Uamsho Z,bar
Jeshi
la Polisi Zanzibar lafanikiwa kuwakamata Viongozi wengine wawili wa
uamsho leo hii mnamo majira takribani saa tano mchana hapo katika
mahakama ya Mwanakwerekwe iliopo walaya ya wiya mjini magharibib unguja,
Kukamatwa kwa viongozi hao kumekuja maara tu baada ya viongozi hao
wa uamsho ambao ni Abdalla Madawa ambae ni katibu wa Uamsho na mwenzake
anaejuulikana kwa jina la Mzee Fikirini kufika katika mahakama hio
wenyewe kwa ajili ya kusikiliza kesi inayowakabili baadhi ya viongozi
wenzao walaioshtakiwa kwa makosa mbali mbali yakiwemo ya uharibifu na
uchafuzi wa mali za Umma, waliofikishwa kwa mara nyengine katika
mahakama ya Mwanakwerekwe kwa ajili ya kuendelea kusomewa kesi zao.
Inaaminika kwamba kukamatwa huko kumekuja baada ya Jeshi la Polisi
Zanzibar kuendelea na msako wa baadhi ya viongozi ambao wamo kwenye
orodha ya watu wanaowatafuta kwa madai walihusika ma vitendo mbali mbali
vya uchafuzi wa amani hapa nchini.
Kwa upande wa Jeshi la Polisi bado hawajasema lolote hadi muda huu
kuhusiana na kukamatwa kwa viongozi hawa lakini tunaendelea kufanya
juhudi ili tujue nini watakisema na wao.
No comments:
Post a Comment