Wednesday, December 26, 2012

Samaki Wafariki kwa mpigo Wambaa kusini Pemba

Bwawa la kufugia Samaki



 
 
 
 
 
 
Rate This
Katibu wa jumuia ya ‘jambo Group Cooperative’ ya kwanzani wambaa Bw: Hafidhi Juma Ali, amesema Samaki wao 2,800 waliokufa hivi karibuni, hawakumwagiwa sumu, bali walisababishwa na Mvua kubwa ilionyesha

Akizungumza na Waandishi wa Habari hizi huko Wambaa, Katibu huyo Amesema awali walidhani kuwa Samaki hao, walikufa kutokana na kumwagiwa sumu, lakini baada ya timu ya wataalamu kuwachunguza walithibtisha kuwa walizidiwa na maji ya mvua na vumbi

Amesema kuwa, kutokana na Mvua ilionyesha hivi karibuni na Bwawa lao kuingia maji hayo, hivyo samaki hao waliingia vumbi kwenye machavu yao na kusababisha kufa kwa umoja

Nae Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Bw: Khamis Shehe Khamis, amewakumbusha Viongozi waliotoa ahadi ya kuwasaidia baada ya kupata hasara hiyo, kutimiza ahadi zao, ili kurejesha hasara walioipata

Bw: khamis aliwapongeza viongozi wote waliofika kwenye jumuia baada ya kupata taarifa hiyo, na kutoa ahadi mbali mbali, hivyo wakati umefika sasa kuzitimiza ili kuendeleza ufugaji huo wa samaki.

Kwa upande wake mjumbe wa Jumuia hiyo Nd: makame Suleiman Makame, amesema kutokana na samaki wao 2,800 aina ya Mwatiko kufa wamepata hasara ya zaidi ya shilingi milion 8

Jumuia ya ‘Jambo Group Cooperative’ ya kwazani wambaa mwaka jana, ilipata hasara ya zaidi ya shilingi Milion 4, baada ya Mboga Mboga zao mbali mbali  ikiwa ni pamoja na matikiti 2,000 (elfu mbili) kuungua kwa jua

NA HAJI NASSOR, PEMBA  

No comments:

Post a Comment