Bakora sio kielelezo cha kumlea mtoto bali bakora ni adhabu kwa watu maalumwenye umri maalum.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi idara shule za maaandalizi ya msingi mhe Uledi Juma Wadi alipokua akiwahutubia walimu na wazazi waliohudhuria katika
iliopo mkunazini yaliofanyika katika ukumbi wa haile sellasie.
Aidha amewaomba walimu na wazazzi kuwafundisha watoto elimu ya kumjua mola wao pamoja na dini yao ili kuweza kuwalea katika mazingira yalio bora katika miaka ya mbele ili kuwa viongozi bora.
Amebainisha ya kwamba shule za binafsi zina umuhimu mkubwa katika jamii kwani zinasaidia kuipunguzia mzigo serikali kwani serikali haina uwezo wa majengo ya kutosha kuwasomesha wazanzibar wote. aidha ameziomba shule nyengine za chekechea kuiga mfano wa taaluma inayotolewa shuleni hapo kwani hakuna malamimiko yeyote yaliofikishwa ofisini kwake yanayohusiana na shule hiyo.
Na katika risala iliosomwa na BI Maimuna kwa niaba ya walimu wenziwe amesema shule yao imeanza na wanafunzi saba lakini kwa sasa ina wanafunzi 270, walimu 11 na madada 8, hivyo amesema changamoto kubwa inayowakabili ni kucheleweshwa kwa wanafunzi wakati wa asubuhi kitu ambacho kina wafanya baadhi ya wanafunzi hao kukosa vipindi vya mwanzo, aidha baadhi ya wazazi hawqahudhurii kikamilifu vikao vinavyoitishwa na shule sambamba na kutokuwasimamia watoto wao wanapopewa kazi za nyumbani {home work}.
Hivyo wamewaomba walezi na wazazi wa wanafunzi hao kuwa makini kwa kujenga ukaribu na walimu ili kuweza kuwaendeleza watoto wao kwani elimu bora ina hitaji mashirikiano ya walimu wazazi na wanafunzi.
No comments:
Post a Comment