Na Adnan Hussein, Mogadishu
Desemba 24, 2012
Karibia miezi sita baada ya kufunguliwa, jengo la huduma ya afya ya
wanyama na kituo cha karantini cha al-Jazira huko Mogadishu
linajitayarisha kusafirisha nje mzigo wa kwanza wa mifugo mwezi Machi,
kwa mujibu wa viongozi.
Mifugo yote katika jengo la huduma inafanyiwa uchunguzi na matibabu ili kuhakikisha inakuwa na viwango vya afya vya kimataifa kabla ya kuidhinishwa na serikali kwa ajili ya kusafirishwa nje ikiwa hai, alisema Mohamed Mohamud, mkurugenzi wa maendeleo ya kilimo katika Wizara ya Maliasili.
Jengo hilo, ambalo lilifunguliwa tarehe 28 Julai katika sherehe iliyohudhuriwa na rais mstaafu Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, linamilikiwa na wawekezaji wa Somalia na linasimamiwa chini ya usimamizi na uangalizi wa Wizara ya Maliasili ya Somalia, alisema.
"Idara yetu ya afya ina kazi ya kusimamia jengo jipya na itaweka karantini kwa wanyama wagonjwa," Mohamud aliiambia Sabahi. "Wanyama waliokufa watachinjwa na ama kuchomwa au kufukiwa ili kuzuia uambukizaji wa wanaosafirishwa."
Mifugo iliyofanyiwa uchunguzi itasafirishwa kupelekwa Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri, alisema, akiongeza kwamba wizara imejitolea kutoa mifugo yenye afya katika bei nzuri za soko.
Jengo hilo lilijengwa kwa miaka mitatu na linaweza kuchukua ng'ombe 250,000. Eneo lina viwanja vya malisho na chombo cha maji kwa ajili ya kondoo, ng'ombe na ngamia, pamoja na huduma ya ukaguzi yenye wafanyakazi wa taaluma ya matibabu ya mifugo na wafanyakazi wasaidizi waliopata mafunzo.
Mradi huo ni sehemu ya shughuli nyingi ambazo serikali inasaidia katika kufufua uchumi wa Somalia.
Waziri wa Maliasili wa Somalia Abdirizaq Omar Mohamed alisema wizara yake inashirikiana kwa juhudi na wawekezaji kuendeleza uzalishaji wa kilimo, kuboresha uhakika wa chakula na kuimarisha usafirishaji nje ya nchi pamoja na wafanyabiashara wabia wa kanda.
Kuwavutia wawekezaji binafsi na kujenga miundombinu inayofaa kwa usafirishaji nje ya nchi wenye mafanikio wa rasilimali za Somalia ni kipaumbele cha wizara, Mohamed aliiambia Sabahi.
"Hivi karibuni tutasheherekea malengo yetu ya kuendelea kiuchumi na [Somalia] siku moja, itaweza kuendele a bila ya kutegemea msaada kutoka nje", alisema.
Mohamed alisema wizara kwa sasa inashirikiana na sekta binafsi kurejesha usafirishaji nje ya nchi wa ndizi, uliyowahi kuwa chanzo cha mapato kwa nchi hiyo.
Waziri aliwataka Wasomali na wafanyabiashara wa kigeni kuwekeza Somalia na kutumia fursa nyingi zilizopo zenye faida kwa ajili ya kuendeleza rasilimali nyingi za nchi.
Deynaba Makaraan Barow, mfugaji mwenye miaka 44 kutoka Shabelle ya Chini, alisema kujihusisha kwa serikali katika kuwezesha na kuendeleza usafirishaji mifugo nje ya nchi ni dalili inayotia moyo.
"Biashara ya mifugo nyakati za serikali kuu ya zamani [kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe] kilikuwa ni chanzo muhimu cha kichocheo cha uchumi kwa nchi," Barow aliiambia Sabahi. Alisema ana matumaini kwamba wafugaji wa Somalia kwa mara nyingine wanaweza kusafirisha nje ya nchi mifugo yao katika kiwango hicho hicho.

No comments:
Post a Comment