Jan
4
2013
Chama cha Wakulima Tanzania AFP
kimesema ipo haja ya kurudishwa kwa sheria ya upimaji wa bidhaa zote
zinazozalishwa na wakulima pamoja na wafugaji nchini kama zinvyopimwa
zile zitokazo nje ya nchi ili kuwezesha kutoa faida kwa mkulima na
kuepusha vitendo vya ulanguzi unaofanywa na baadhi ya wafanya biashara.
Katika taarifa yake Mkurugenzi
wa Mipango na Sera wa AFP Rashid Mchenga iliyosambazwa kwa vyombo vya
habari ameelza kwamba kutokupimwa kwa bidhaa hizo kunapelekea
ubabaishaji unaofanywa na baadhi ya walanguzi wachache kwa kunufaika na
mazao yanayozalishwa na wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi kwa kuwapa
bei ndogo na kuwazidishia wauzaji wa madukani na magengeni pamoja na
walaji.
Amesema kuwa kutokuwa na
mipango mizuri ya uendeshaji wa masoko sambamba na kutofuata sheria za
masoko ndio chanzo kikubwa cha kutomlinda Mkulima, mfugaji na mvuvi kwa
mujibu wa sheria hivyo iko haja ya seriksli zote mbili za SMZ na SMT
kuanzisha na kudumisha sheria za kumlinda mkulima, mfugaji na mvuvi kwa
kupimwa mazao yao na kuuzwa kwa kutumia mizani.
Amesema kuwa sheria ya upimaji
wa mazao kama muhogo, ndizi, viazi na mazao mengine yaanze kupimwa
kuanzia kwa wakulima wenyewe ili kujua bei ya mkulima mwenyewe wafanya
biashara na walaji sambamba na wafugaji na wavuvi ili kuwezesha haki
kutendeka kwa mujibu wa sheria ya haki ya mkulima.
Amesema kuwa sheria za upimaji
wa vyakula pamoja na mazao mengine zilikuwepo kuanzia miaka ya 74-80
hivyo hapana budi kwa serikali kuzirejesha sheria hizi ili kumjengea
mustakbali mzuri mkulima.
Amesema kuwa upimaji wa bidhaa
kwa kutumia mizani kutaisadia serikali katika kupanga bajeti yake vizuri
kwa kujua hesabu zake za matumizi ya siku,wiki, mwezi na mwaka pamoja
na kujua matumizi ya taifa na watu wake kwa kuendana na bajeti
iliyopangwa.
Aidha amewataka wakulima,
kujipanga ili kuondokana na walanguzi wa masokoni na mashambani
waliojitokeza siku hizi kununua mazao machanga mashambani na badala yake
wasubiri yapevuke ili waweze kuuza kwa faida na sio kwa hasara na wauze
kwa mujibu wa sheria.
Pia amewataka wananchi wafuate
sheria za kilimo, mifugo na uvuvi ili kuweza kupata maendeleo yao na
serikali zote mbili ziwasaidie wakulima, wafugajib na wavuvi kwa
kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili ili kutekeleza dhana halisi
ya kilimo kwanza na mapinduzi ya kilimo na maendeleo ya mifugo na uvuvi
kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment