Balozi mdogo wa Msumbiji aliepo
Zanzibar Bw, Bernado Constantino Lidimba amewataka Watanzania na
Wanamsumbiji kuyaendeleza mashirikiano ya kiuchumi na kijamii yaliyopo
baina ya nchi hizo ili kuuendeleza uhusiano uliojengeka kwa muda mrefu.
Ameyasema hayo katika hafla ya
kuagana na wana jumuia ya Tanzania and Mozambique Friendship Association
(TAMOFA) iliofanyika katika ofisi ya Ubalozi mdogo wa Msumbiji uliopo
Kikwajuni mjini Zanzibar.
Amesema kuwa mahusiano hayo
yalioasisiwa na marasi wa kwanza wa nchi hzo yanalengo la kujenga udugu
miongoni mwa nhi hizo hivyo hapana budi kuyaendeleza mashirikiano hayo.
Amesema kuwa katika
kuyaendeleza mashirikiano haya serikali za Tanzania na Msumbiji zimekuwa
na tabia ya kubadilishana wanafunzi wa vyuo vikuu ili kuaendeleza
mashirikiano hayo hadi katika nyanja za kielimu.
Aidha Bw. Lidimba ameahidi kuwa balozi mzuri wa TAMOFA huko
aendako, pia amewataka wanajumuia hao kujenga utamaduni wa kushirikiana
na wananchi wengine wa Tanzania walioko Msumbiji kuweza kujiunga na
jumuia hiyo ili kukuza mashirikiano hayo miongoni mwao.
Katika risala yao wanajumia ya TAMOFA walioiwasilisha kwa balozi
huyo wameelezea kusikitishwa kwao kwa kumaliza muda wake nchini kwani
amekuwa na msaada mkubwa kwa jumuia hiyo hivyo kumtaka aendelee
kushirikiana nao pale watakapo hitaji ushirikiano wake.
Pia wamemtakia kheri na fanaka katika misha yake pamoja utendaji mwema wa kazi zake pale atakapo pangiwa kuendelea kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment