Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ili huduma za
maji safi na salama ziendelee kudumu kizazi cha sasa kinapaswa
kuzingatia utunzaji wa mazingira samba na kuheshimu miundo mbinu ili
sekta hiyo itowe huduma kiuhakika.
Balozi
Seif alieleza hayo wakati akizindua mradi wa Maji safi na salama wa
Michenzani hadi chokocho uliojumuisha visiwa vidogo vidogo vya vilivyomo
pembezoni mwa Jimbo la Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini
Pemba.
Uzinduzi
huo unaotarajiwa kuhudumia zaidi ya wakazi wa 21,841 wa Vijiji vya
Mkanyageni, Chokocho,Michenzani, Kisiwa Panza na Makoongwe ni miongoni
mwa shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 49 ya Mapinduzi
matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Balozi Seif alisema wakati
umefika kwa Wananchi kushirikiana na Serikali sambamba na Viongozi wao
wa jimbo kuendesha kampeni ya upandaji miti ili rasilmaliya maji
iliyobarikiwa nchi iweze kudumu kwa muda mrefu.
“
Hii tabia iliyozoeleka hapa kwetu ya mtu kukuta mfenesi twende, muembe
twende, au mti wowote twende kwa ushawishi wa msumeno wa Moto kwa kweli
imetufikisha pabaya na tunapaswa kuwa na tahadhari na tabia hii mbaya”.
Alifafanua Balozi Seif.
Alifahamisha kwamba licha ya juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na
Serikali za kumarisha huduma za maji lakini bado sekta hii inaonekana
kuharibiwa kwa makusudi na baadhi ya watu na isipodhibitiwa upungufu wa
huduma hii utegemewe kuongezeka.Balozi Seif aliwaasa wabunge na wawakilishi kuwa waangalifu katika kutambua mahitaji ya wananachi wanaowaongoza katika suala zima la kuimarisha miradi ya kiuchumi na maendeleo.
Usimamizi wa maendeleo ya Jimbo umo ndani ya usimamizi wa wabunge na wawakilishi ambao ndio waliokubali kubeba jukumu hilo muhimu la kuwatumikia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimshukuru na kumpongeza Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye ni mzaliwa na Jimbo la Mkanyageni Pemba kwa juhudi zake za kupigania maendeleo ya jimbo hilo.
Balozi Seif alisema kitendo cha Profesa Mbarawa cha kutekeleza ahadi alizotowa wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 licha ya kukosa fursa ya kuliongoza jimbo hilo katika wadhifa wa Mbunge lakini alionyesha ushujaa kwa kukamilisha ahadi hizo.
“ Profesa Makame Mnyaa Mbarawa anafaa kupongezwa na jamii yote kwa uungwana wake wa kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni licha ya k
ukosa fursa aliyoiomba ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Mkanyageni”. Alionyesha furaha yake Balozi Seif.
Aidha aliwaeleza wananchi hao wa Jimbo la Mkanyageni kwamba Serikali kupitia mamlaka ya Maji { ZAWA } imeshasambaza huduma za Maji safi na salama kwa zaidi ya asilimia 89%.
Aliipongeza mamlaka ya maji kwa jitihada zake za kusambaza huduma ya maji mjini na vijijini.
Mapema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Madini Nd. Mustafa Aboud Jumbe alisema lengo la Serikali kupitia Wizara hiyo ni kuwaondoshea kero ya Wananchi ili wapate fursa ya kushiriki vyema katika harakati za Maendeleo.
Nd.
Mustafa alisema mradi wa maji safi na salama wa Michenzani hadi
Chokocho ambao ni miongoni mwa juhudi hizo itasaidia kuwaondoshea
wakaazi wa maeneo hayo wapatao 21,841.
Alisema
mradi huo ulioanza harakati za matengenezo mwezi Julai mwaka 2011 na
kumalizika mwezi Septemba mwaka 2012 umehusisha Visima Viwili
vitakavyosambaza maji katika Vituo viwili vikubwa katika eneo hilo.
Akitoa
shukrani zake Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Profesa Makame Mnyaa Mbarawa alisema chimbuko la
mradi huo lilianza wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Aliwaasa Wananachi wa Jimbo hilo kuacha kubeza maendeleo
wanayopelekewa ambayo mengine ni ahadi zilizotolewa ambazo hazina budi
kutekelezwa na wale walioshiba uungwana.
Mradi
wa Maji safi na salama wa Michenzani hadi Chokocho umegharimu jumla ya
shilingi za Kitanzania Milioni 120,535,224/- ambazo kati ya hizo Profesa
Makame Mnyaa Mbarawa ametoa shilingi Milioni 73,000,000/-
Profesa
Mbarawa pia akakabidhi mabomba na Mipira ya maji ili kusambazia maji
katika vijiji hivyo vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 23,000,000/-.
No comments:
Post a Comment