POLISI nchini wametangaza kupokea bunduki 439 na risasi 37 kutoka kwa
watu waliozisalimisha kutokana na wito uliotolewa na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi mwezi mmoja uliopita kuwataka wenye
silaha kinyume cha sheria wazisalimishe.
Miongoni mwa silaha zilizosalimishwa na watu hao ni pamoja na shortgun
(29), gobore (352), SMG (11), Riffle (20), bastora (22), Airgun (1),
Rocket launcher (2) na SAR (2).
Msemaji wa polisi , Advera Senso alisema katika taarifa yake kwa vyombo
vya habari jana kwamba kupatikana kwa silaha hizo ni ushirikiano mzuri
kati ya polisi na wananchi.
Senso alisema polisi wamejipanga kwa kufanya operesheni maalumu itakayoendeshwa nchi nzima kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na raia wema ili kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.

Alisema operesheni hiyo itafanyika kutokana na kumalizika kwa muda
maalumu alioutoa Waziri Nchimbi kwa watu wenye silaha kuzisalimisha bila
masharti yoyote.
Hata hivyo taarifa ya Senso haikutaja ni lini operesheni ya kusaka bunduki itaanza nchini.
Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za mtu ama kikundi cha watu wanaosadikiwa kujihusisha na umiliki wa silaha isivyo halali au matukio ya uhalifu wa aina yoyote ile ili kuhakikisha uhalifu wa kutumia silaha unapungua.”

Senso alibainisha kwamba mtu yeyote atakayetoa taarifa za mafanikio
zitakazowezesha kukamatwa kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria
watazawadiwa Sh100,000 kulingana na mafanikio ya taarifa aliyoitoa.
CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment