Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi ameitaka wizara ya Habari utamaduni utalii na Michezo kutoa ufafanuzi kwa raiya kuhusiana na suala zima la matangazo kupitia mfumo mpya wa Digital kutokana na jamii kutokua na uelewa juu ya mfumo huo mpya.
Dk:Shein ameyasema hayo wakati alipokua akizindua rasmi ufunguzi wa mradi mpya wa matangazo kupitia digital huko Rahaleo wilaya ya mjini unguja.
Dk;Shein amesema kuwa Jamii Nchini imekua ikijiuliza maswali mengi juu ya mfumo mpya wa matangazo unaozungumziwa hivi sasa pasipo na kuelewa chochote ,wana imani kwamba tv zao za zamani zitakuwa hazifai kutumiwa tena na wanunue tv mpya jambo ambalo sio sahihi,hivyo basi wanahitaji kuelimishwa ipasavyo kwa lengo kupata ufahamu juu ya mfumo huo.
Sambamba na hayo,amelitaka shirika la habari Zanzibar(ZBC)kufanya kazi ipasavyo ili kuenda sambamba na mahitaji ya wananchi na taifa kwa ujumla,kama yalivo mashirika mengine ulimwengini,ameshangazwa na kuwa ZBC ilikuwa ndio tv ya mwanzo ya rangi Afika mashariki lakini sasa imekua ndio ya mwisho kutokana na utendaji wake.
Pia amezibainisha baadhi ya changamoto zinazolikabili shirika hilo kua ni pamoja na uendeshaji mbovu wa vipindi visivyo na mahitaji kwa jamii,pia amesema kumekuwa na tatizo la kuendesha vipindi vya habari kwa muda usio sahihi kama ilivopangwa.
Hivyo Dk;Shein , amemtaka Waziri wa habari Utamaduni Utalii na michezo pamoja na Katibu wake kuhakikisha kua kazi inatendeka ipasavyo ili kulinda mahitaji ya wanachi kupitia ZBC.
Aidha amesema kuwa yeye amekuwa akiwachagua watu wenye sifa ili kuendesha shirika hilo lakini anashangazwa na maneno yanayosemwa na baadhi ya watu kuwa amekuwa akichagua rafiki zake lakini suala hilo sio sahihi kwani angemchagua mwanawe ambae pia kasomea masuala ya habari.
Sambamba na hayo ameiagiza wizara ya habari kuliangalia upya suala la kuwafungia wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar kwani vijana wamekuwa na makosa mengi hivyo basi si vyema kutumia jazba dhidi yao badala yake njia ya busara itumike na kumaliza tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment