Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya Seagull transport ltd, Said Abdulrahman Juma, wakati akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake kokoni mjini Zanzibar.
Amesema serikali imechukua uamuzi wa kusimamisha huduma za kibiashara na usafirishaji wa abiria kwa boti ya mv. Kalama kwa muda mrefu bila ya kufuata taratibu za kisheria jambo alilodai linaisababishia hasara kubwa kampuni hiyo.
Bw.said amesema serikali ilitangaza kupiga marufuku boti ya MV Kalama inayofanana kwa kila hali na boti ya mv. Skagit iliyozama mwezi julai mwaka jana, iliyobainika haifai kusafirisha abiria kwa umbali mrefu.
Aidha amefahamisha kuwa kampuni hiyo inaendeshwa na wawekezaji wazalendo, cha kushangaza uamuzi huo ulitolewa bila ya kufanya ukaguzi wala kupitia historia na michoro ya meli tokea ilipotengenezwa.
Aidha ameiomba serikali kupitia mamlaka ya vyombo vya usafiri wa baharini Zanzibar- ZMA, kushirikiana na kampuni hiyo kutafuta wakaguzi kutoka katika makampuni ya kimataifa ili kuifanyia ukaguzi wa kina meli hiyo.
Alisema toka kusimama kwa huduma za meli hiyo yenye uwezo wa kuchukua abiria 300 na tani 200 za mizigo, kumesababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni tatu, jambo alilosema linazorotesha uendeshaji wa kampuni hiyo.
Naye meneja masoko wa kampuni hiyo Sadiki Khamis, alisema kampuni inategemea mikopo ya benki ambapo mpaka sasa, wanadaiwa riba ya shilingi bilioni 2.2, ambazo kampuni haina uwezo wa kulipa.
Hata hivyo, amesema kuwa wamefanya taratibu za kuwasiliana kwa njia ya barua na simu na watendaji husika ili wazungumze hatima ya utendaji wa meli hiyo lakini juhudi hizo hazijafanikiwa kwani wahusika wanasema wametingwa na majukumu ya kiutendaji.
No comments:
Post a Comment