Wednesday, January 23, 2013

SMZ YAFANIKIWA MITARO YA MAJI MACHAFU


 
 
 
 
 
 
Rate This

Imewekwa na Hamed Mazrouy

ImageWaziri wa Nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Mwijihaji Makame
ImageWaziri wa Nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Mwijihaji Makame

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Mwijihaji Makame amesema lengo la kujengwa mtaro wa maji ya mvua wenye urefu wa mita Miasaba kutoka block namba 5 na namba 10 kuelekea msikiti mabati ni kusaidia kupokea maji ya mvua yanayotokea barabara ya Michenzani na mitaa ya jirani ili kuyapeleka bondeni kisiwandui kuelekea pwani.
Akijibu swali katika kikao cha Baraza la Wakilishi aesema malengo ya kuchimbwa kwa mtaro yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani kiwango kikubwa cha majiya mvua yanaingia katika mtaro huo licha ya kukumbwa na changamoto ndogo ndogo za kuingia mchanga na uchafu mwengine.
Aidha amesma kuwa ujenzi wa mtaro huo ulikuwa ni sehemu ya mradi wa michirizi wa awamu ya pili mradi ambao umetekelezwa chini ya ufadhili wa serikali ya Ujarumani na kugharimu jumla ya shilingi milioni 148.8.
Pia ametoa wito kwa wananchi wanaokaa maeneo hayo kutoa ushirikiano wao katika kuuweka mtaro huo katika hali ya usafi pamoja na kuiwataka viongozi wa eneo hilo wakiwemo Wawakilishi, Wabunge, Madiwani pamoja na Masheha kusidia kuwashajiisha wananchi umuhimu wa kuweka hali ya usafi ndani yam taro huo.
 Dk, Mwinyihaji amesema kuwa Bareaza la mamispaa la mji wa Zanzibar linachukua jitihada za kuyajenga upya mafuniko yanayovunjika au yanapoibiwa kwa kuyapa kipaumbele maeneo hatarishi zaidi kulingana na uwezo uliopo kwa lengo la kuepuka maafa ytanayoweza kujitokeza.

No comments:

Post a Comment