Imewekwa na Hamed Mazrouy
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein ametakiwa kuchukua hatua
madhubuti za kuwawajibisha watendaji wa Serikali wenye kufanya
ubadhirifu wa fedha na kuisababisha Serikali hasara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na
Mashirika, Baraza la Wawakilishi, Omar Ali Shehe alitoa ushauri huo
wakati akifanya majumuisho ya maoni na michango ya wajumbe wa baraza
hilo yaliyotolewa wakati wa kuchangia ripoti ya kamati hiyo.
Shehe alisema, Dk Shein anatakiwa kuwa jasiri na kujiamini katika
uchukuaji wa hatua kama anavyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Kikwete ambaye amewawajibisha viongozi mbalimbali
wakiwemo mawaziri kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha serikalini.
“Bahati nzuri Mheshimiwa Kikwete anafuata sera za Chama Cha Mapinduzi na Dk Shein pia anafuata sera na kanuni za chama hicho kwa hivyo namwomba sana Dk Shein afuate na aige mfano anaouchukua Mwenyekiti wake,” alisema.

Wakitoa maoni yao wawakilishi walitaka Serikali kuchukua hatua
kutokana na fedha nyingi za Serikali kupotea bila ya wahusika
kuchukuliwa hatua licha ya ripoti hizo kutoa mapendekezo kadhaa.
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Mahmoud Mussa Abdallah (CCM),
alisema anakubaliana na ripoti hiyo iliyowasilishwa lakini bado
kunahitajika kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wahusika na kuona vyombo
vya sheria vitakavyolishughulikia suala hilo kuwa makini katika
kuifanyia kazi ripoti hiyo.
Alisema Zanzibar inafuata utawala bora na haitakuwa busara kuona kazi
kubwa iliyofanywa na kamati hiyo ikaachwa bila ya kuchukuliwa hatua
kwa watendaji waliotajwa katika ripoti hiyo.
Mwakilishi huyo alisema ni kweli ndani ya Shirika la Umeme Zanzibar
kumekuwa na matatizo na waliofanya hivyo hawakutumwa na vyama vyao kwani
ndani ya CCM inakataza wala rushwa na wezi na ni vyema Serikali
ikawachukulia hatua za kisheria wahusika wote.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu, alisema Serikali bado haijaonyesha umakini na hivyo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wana haki ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Serikali kutokana na kutokuwana hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika wa ubadhirifu wa mabillioni ya fedha.

Alisema wajumbe wa baraza hilo waone kuwa, wanaendelea kufanya kazi
ya kuwatumikia zaidi wananchi kwa kuelezea mambo wanayoyataka yakiwemo
kufichua mambo maovu yanayotokea.
Jussa alisema wakuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wapo wenye
kutumia huduma ya umeme bila ya kulipia jambo ambalo gharama zao
hulipishwa wananchi wanyonge. Hiyo inaweza kuwa ni hatari kwa taifa huku
akitahadharisha kuwepo kwa matabaka.Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni, Salmin Awadh Salmin (CCM), akitoa maelezo yake alisema anasikitishwa na Ofisi ya Mdhibiti wa Serikali kuona imeshindwa kubaini ubadhirifu huo uliotokea katika shirika hilo.
No comments:
Post a Comment