Thursday, January 17, 2013

Mamlaka yenye tahadhari baada ya al-Shabaab, wanamgambo wa Uganda kujiunga na vikosi

Wanamgambo wa al-Shabaab nchini Somalia na waasi wa Uganda wa Vikosi Shirika vya Kidemokrasia (ADF) wamekuwa na uhusiano wa ushirikiano angalau kwa mwaka mmoja sasa, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.
  • Askari kutoka Kikosi cha Ulinzi cha Watu wa Uganda wakipiga doria karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kupambana na Vikosi Shirika vya Kidemokrasia mwezi Machi 2007. [Peter Busomoke/AFP] Askari kutoka Kikosi cha Ulinzi cha Watu wa Uganda wakipiga doria karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kupambana na Vikosi Shirika vya Kidemokrasia mwezi Machi 2007. [Peter Busomoke/AFP]
Ripoti hiyo, iliyotolewa na Kikundi cha Wataalamu cha Umoja wa Mataifa kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi Novemba 2012, ilisema kulikuwa na "mifano kadhaa ambayo inaunga mkono utetezi wa serikali ya Uganda kwamba ADF ina uhusiano na al-Shabaab nchini Somalia".
"Kwa mujibu wa wapiganaji wa zamani, ADF iliwapa mafunzo watu vijana katika kambi zao kwa miezi kadhaa kabla ya kuwapeleka nchini Somalia kupigana," ripoti hiyo ilisema. "Kikundi cha kwanza cha vikundi hivi kiliondoka katika kambi hiyo mwezi Novemba 2011."
ADF ni shirikisho la madhehebu ya Kiislamu na vikosi vya upinzani vinavyopinga serikali ya Uganda. Kwa asili vilianzia Magharibi mwa Uganda, ADF kwa sasa inafanya shughuli zake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na inachukuliwa kama asasi ya kigaidi.
ADF na washirika wake wa ndani walihusika na mashambulio kadhaa ya ndani mwishoni mwa miaka ya 1990, lakini wamekuwa hawana nguvu kwa miaka ya hivi karibuni. Kwa hiyo, uthibitisho kwamba imeungana na vikundi vingine vya kigaidi vya kikanda, kama vile al-Shabaab, mamlaka zinapaswa kuwa na tahadhari.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa imethibitisha kwamba mwezi Novemba 2011, wakala wa al-Shabaab walituma dhamana kwa kijana wa kiume wa kiongozi mkuu wa ADF Jamil Mukulu baada ya kukamatwa jijini Nairobi, na walimsaidia na familia yake. "Shirika la Upelelezi la Kenya lilikiambia kikundi hiki kuwa wanamiliki rekodi ya mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Mukulu na wakala wa al-Shabaab mwenye makaazi Eastleigh," ripoti hiyo ilisema.
Kapteni mstaafu wa kikosi cha anga cha Kenya Simiyu Werunga, mkurugenzi wa Kituo cha Afrika cha Mafunzo ya Usalama na Mikakati jijini Nairobi, alisema al-Shabaab wanajaribu kutafuta muungano na vikundi vingine vya wanamgambo kwa jitihada ya mwisho kabisa.
Al-Shabaab inatafuta uhusiano na vikundi vingine kuwaonyesha wanaowaonea huruma kuwa "bado wako imara na wanakua, ambapo siyo kweli", alisema.

Washirika wa Al-Shabaab

Huu sio wakati pekee ambapo al-Shabaab imejaribu kujihusisha yenyewe na vikundi vingine vya wanamgambo vya Afrika. Mwaka 2011, kikundi cha wanamgambo kilijihusisha chenyewe na Boko Haram cha Nigeria, na pia kinatuhumiwa kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa Nigeria nchini Somalia.
Ushirikiano ulikuwa wa muda mfupi kutokana na maandalizi hafifu na masuala ya kilojistiki kama vile umbali kati ya ngome ya al-Shabaab katika Afrika Mashariki na Boko Haram huko Afrika Magharibi, Werunga alisema.
Hata hivyo, umbali kati ya ADF na al-Shabaab unaweza kuwa wa kumudu zaidi na unaweza kuwapa wapiganaji fursa ya kuwasiliana na kupanga njama kwa usumbufu kidogo, alisema Gideon Maina, mwanasheria na profesa wa sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
Alisema vikundi vyote vinaifahamu Nairobi na vinaweza kuifanya kwa urahisi kuwa kitovu cha jitihada zao za pamoja. "Hili linapaswa kuwa jambo la kuzingatia kwa kanda yote ya Afrika Mashariki kwa sababu [vikundi hivi] vinaweza kubadilika kwa kuingiza watu wapya wanaowaonea huruma kutoka katika kanda," Maina aliiambia Sabahi.
"Ni juu ya [serikali] mkoani pamoja na mfumo wake wa usalama kufanya kazi kwa bidii kutambua na kuwasambaratisha kabla ya kufikia silaha zaidi na kuunda mtandao wa kazi mkoani," alisema Maina, akiomba viongozi kufanya kazi kwa pamoja ili kuanzisha jeshi la pamoja la kuzuia ugaidi na kuimarisha doria ya mipakani ili kuzuia silaha za magendo.
Mustafa Yusuf Ali, katibu mkuu wa Baraza la Afrika la Viongozi wa Dini, alisema wapiganaji wa al-Shabaab wanatawanyika katika kanda yote kuepuka kukamatwa na vikosi vya ulinzi.
"Vikundi huria kama al-Shabaab vinajitahidi kujiongeza na kutumia kikamilifu mwanya wa kutofanana katika mbinu zao, kutumia ujanja na harakati ili kubakia kuwa muhimu," aliiambia Sabahi.
Hata hivyo, Ali alisema tatizo kubwa linalohusiana na ugaidi katika kanda sio uhusiano "mpya" kati ya al-Shabaab na ADF, bali kutokuwa na uwezo kwa mashirika ya ulinzi katika Pembe ya Afrika wa kukabiliana na ugaidi kwa utaratibu.
Uongozi hauwezi kuvizuia kabisa vikundi hivi visiungane, alisema, lakini wanaweza kusaidiana kupunguza kufaa kwao kwa kipindi kifupi kwa kushirikiana upelelezi na katika kipindi kirefu kwa kupata ushawishi na mawazo ya umma katika hatari ya kuwa na siasa kali.
"Kumbuka, vita hivyo havihusu kushinda maeneo au [kuangamiza] adui, bali kuhusu [kushinda] nafsi za watu," Ali alisema.

Viongozi wa Tanzania katika tahadhari

ADF pia inaendesha vituo vya msaada wa kifedha kutoka katika bandari nchini Tanzania na Kenya, ripoti ya Umoja wa Mataifa ilieleza.
"Kwa mujibu wa wapiganaji wa zamani, rasilimali za fedha zilizotokana na usafiri zilizalishwa na vituo hivyo kwa ADF kutokana na kuvuka kupitia mpaka wa Kasindi kutoka Uganda kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo," ripoti ilieleza. "ADF pia inazalisha mapato ya ndani kwa biashara mbalimbali katika himaya ya Beni."
Wapiganaji hao, viongozi wa nchi na mamlaka za Uganda waliiambia Kundi kwamba ADF inapata faida kutokana na uzalishaji haramu wa mbao na migodi kadhaa ya dhahabu.
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, mamlaka za Kenya ziliiambia Kundi kwamba wanaamini Kiongozi mkuu wa ADF Mukulu kwa sasa anaishi Tanzania.
Viongozi wa Tanzania walisema wanafuatilia hali na wako katika tahadhari kubwa kwa tukio lolote la kutia wasiwasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Constantine Masawe alisema polisi wamekua wakiangalia kiintelijensia kwamba wanapendekeza ADF inaendesha kituo cha msaada wa kifedha katika bandari ya Tanga, pamoja na huko Bujumbura, Kigali na Nairobi nchini Kenya.
Alisema intelijensia ya awali ilionyesha kwamba ADF ilikuwa ikipeleka fedha Tanga badala ya kupitisha kutoka bandarini kama ripoti ya Umoja wa Mataifa ilivyoeleza.
"Tunaelewa Tanga ni eneo hatarishi kuhusiana na ugaidi kutokana na hali yake ya kijiografia. Tunapakana na Mombasa ambalo ni korido [la magaidi]," Masawe aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba serikali ilikuwa ikifuatilia taarifa zote zinazoongoza.

No comments:

Post a Comment