Monday, January 28, 2013

Mkutano wa AU kujadili hali nchini Mali

 28 Januari, 2013 - Saa 07:18 GMT
Bi Zuma anaongoza mkutano huu ambao utazungumzia hali ya 
usalama barani Afrika

Mkutano wa Umoja wa Afrika umeanza mjini Addis Ababa, Ethiopia, huku swala la usalama nchini Mali likitazamiwa kupewa kipaombele katika mkutano huo.
Mataifa zaidi barani afrika yanatazamiwa kukubali kuongeza idadi ya mafisa wa kuimarisha usalama nchini Mali .
Akizungumza katika kongamano hilo mwenyekiti wa kamati maalum ya muungano huo - Nkosazana Dlamini-Zuma alisema kuwa mataifa ya bara Afrika nilazima yachukue hatua thabiti kukabiliana na swala la waasi na wanamgambo wenye nia ya kunyakuwa mamlaka kutoka kwa serikali halali
Aliongeza kuwa hatua zaidi zinahitajika kuweza kusuluhisha migogoro mipya na ile ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda katika nchi kadhaa.
Alisema kuwa bara hili haliwezi kustawi na kuafikia malengo ya raia wake bila amani na usalama.
Mkutano huo wa ishirini, ulianza vikao vyake kwa kumkumbuka kwa dakika moja aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Meles Zenawi pamoja na raliyekuwa rais wa Ghana John Atta Mills, aliyefariki mwaka jana.
Mkutano huu utakeoendelea leo, utagusia zaidi vita kati ya wapiganaji wa kiisilamu na majeshi ya kigeni nchini Mali. Pia watazungumzia uwezekano wa kuongeza idadi ya wanajeshi wa nchi za Afrika nchini humo.
Jeshi la Mali likisaidiwa na wanajeshi wa Ufaransa, wanapambana na wapiganaji wa kiisilamu walioteka eneo la Kaskazini mwa Mali kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwaka jana.

No comments:

Post a Comment