Uingereza imewashauri wananchi wake waondoke Somaliland kwa sababu za usalama.
nafikiriwa kuwa kuna Waingereza wachache tu katika eneo hilo, wengi wao wafanyakazi wa mashirika ya misaada, lakini wengine wenye uraia wa Somalia na Uingereza wanasafiri baina ya Uingereza na Somaliland.
Siku kadha zilizopita, Uingereza na mataifa mengine ya Ulaya yalionya raia wake mjini Banghazi, Libya, kuhusu tishio linalowakabili.
No comments:
Post a Comment