Friday, January 25, 2013

Odinga yuko mbele ya Kenyatta katika kura ya maoni ya urais

Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, anaongoza kwenye kinyang'anyiro cha urais mbele ya mpinzani wake mkuu, Uhuru Kenyatta, kwa mujibu wa matokeo ya kura za maoni yaliyotolewa na kampuni ya Ipsos Synovate hapo Ijumaa (tarehe 25 Januari).
Coalition for Reforms and Democracy ya Odinga inaongoza kwa asilimia 46, ikifuatiwa na wa Jubilee Coalition inaoongozwa na Kenyatta na asilimia 40, liliripoti gazeti la Daily Nation la Kenya. Ipsos Synovate ilikusanya maoni ya wapiga kura waliosajiliwa 5,895 katika wilaya 47 kati ya tarehe 12 na 20 Januari.
Kinyang'anyiro hicho kinaonesha uwezekano wa uchaguzi wa marudio, kwani wagombea wanahitaji asilimia 51 ya kura zote kushinda urais.
Muungano wa Amani unaoongozwa na Musalia Mudavadi ulipata asilimia 5 huku ule wa Narc Kenya wa Martha Karua na Kenya National Congress wa Peter Kenneth wakipata asilimia 1 kila mmoja.
Asilimia tano ya wapiga kura walisema hawajaamua.

No comments:

Post a Comment