Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliahidi hapo Alhamisi (tarehe
24 Januari) kwamba serikali yake itapambana na "maovu matatu" ya mauaji,
ubakaji na ufisadi, uliripoti Garowe Online ya Somalia.
Alizungumza katika hoteli ya City Palace mjini Mogadishu katika hafla ya kusherehekea hatua ya Marekani kuitambua serikali ya Somalia.
"Tutapambana na maovu yote matatu ya mauaji, ubakaji na ufisadi,"
alisema. "Serikali yangu haitavumilia kuona watu wasio hatia wakiuawa au
wanawake wakibakwa."
Mohamud alirejelea onyo lake la mwezi Novemba 2012,
akisema kwamba ingawa wanajeshi wa Somalia wanafanya kazi nzuri,
serikali itawachukulia hatua kali sana wale wachache wanaofanya matendo
ya uhalifu.
Rais huyo pia alisema kwamba Wizara ya Fedha na ofisi ya rais si
mafisadi, lakini maafisa wake wachache wanaweza kuwa. "Nawatolea wito
wananchi wasiwafiche maafisa mafisadi," alisema.
Hii ni hafla ya ya kwanza ya Mohamud hadharani tangu arudi kutoka ziara yake ya Marekani.
No comments:
Post a Comment