Kutoka kuondolewa kwa al-Shabaab jijini Mogadishu mwezi Agosti 2011, shughuli ambazo zilikuwa zimepigwa marufuku, kama vile sanaa na michezo, zimerejea katika jiji hilo.
Sanaa za Shik Shik, mojawapo ya studio kubwa za sanaa jijini
Mogadishu, ilifungwa wakati wa utawala wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu
na al-Shabaab, lakini sasa zimeanza kuhuisha maisha, ishara ya
urejeshaji wa utamaduni kadri usalama katika jiji hilo unavyoimarika.
Ilianzishwa na baba yao mwaka 1960, studio hiyo ya sanaa kwa sasa
inamilikiwa na vijana wa kiume watano ambao wanatengeneza aina tofauti
za sanaa. Ambayo iko katika njia panda yenye msongamano wa watu katika
mtaa wa Kilometa 4 ya wilaya ya Hodan ya Mogadishu, duka hili pia huwapa
mafunzo watu katika sanaa na usanifu.
Sabahi walikaa na mmliliki mshiriki Mohamed Hussein Sidow kujadili
utamaduni wa Somalia na jinsi ya kuboresha hali ya usalama inavyodhuru
matukio ya sanaa huko Somalia.
Sabahi: Je, kwa vipi sanaa na kazi za mikono zinavyochangia katika utamaduni na historia ya Somalia?
Mohamed Hussein Sidow: Sanaa na kazi za mikono ni vitu viwili
muhimu zaidi katika historia na utamaduni kwa sababu kama vitu hivi
viwili vitaendelea, utamaduni pia utaongezeka. Sanaa itakufundisheni
kile ambacho watu wa kale walifanya au kutumia.
Sanaa tunayofanya imetokana na utamaduni. Bibi yangu mzaa baba Fadumo
Abdo Salah alikuwa msanii na alimfundisha baba yangu. Bibi yangu
alitengeneza sanaa mbalimbali, kama vile nguo zetu za kuvaa tulipokuwa
wadogo. Alitengeneza masweta na kofia zetu kwa mkono. Ninaweza kusema
tulirithi sanaa hiyo kutoka kwa bibi yetu Fadumo.
Sabahi: Lini ulipoendelea na biashara ya baba yako?
Sidow: Baba yangu aliondoka Mogadishu katikati ya mwaka 2006.
Kimsingi tuliendelea na biashara kabla ya hapo, kwani baba yetu alikuwa
mzee, lakini alikuwa bado anasimamia kazi hiyo.
Sabahi: Tofauti na Sanaa za Shik Shik, kuna studio za sanaa nyingine huko Somalia?
Sidow: Ndiyo, kuna studio za sanaa nyingine huko Mogadishu
zinazomilikiwa na watu waliofundishwa na baba yangu. Ninaamini kwamba
sanaa nchini Somalia itaongezeka kama kutakuwa na amani. Kila kitu
kinategemea amani na kutakuwa hakuna sanaa bila kuwa na amani.
Sabahi: Je, uagizaji mkubwa zaidi za sanaa yenu zinatoka wapi?
Sidow: Uagizaji wetu mkubwa unatoka kwa wafanyabiashara
mbalimbali na mashirika yanayopenda picha zilizochorwa kwa mkono.
Tunapata pia oda kutoka kwa wafanyabiashara wa Somalia wanaorejea kutoka
Uingereza, Uholanzi, Sweden na nchi nyingine zenye watu wengi wa
Somalia. Wanatoa oda za bidhaa za ubunifu wa kimila na za kiutamaduni.
Pia tunabuni alama za madukani na fulana za michezo, kofia na nguo
zilizochapishwa pamoja na bendera yetu zinazoweza kuvaliwa na wote
wanaume na wanawake. Tunatengeneza pia picha za ubunifu wa kimila na
kiutamaduni za watu wetu kama vile silaha (mikuki, ngao na mishale),
mavazi ya kimilana vitu vingine walivyovitumia, pamoja na aina nyingi za
wanyama.
Sabahi: Mnapanga kupanua Sanaa za Shik Shik huko mbele?
Sidow: Kwa sasa tunaendesha studio mbili mjini Mogadishu, na
tunataka kufungua ya tatu mwanzoni mwa mwaka 2013. Pia tunataka
kuimarisha sanaa yetu na kutengeneza vitabu vyenye mambo ya utamaduni wa
Somalia ili kizazi kijacho kiwe na sehemu ya kujifunza kuhusu mila zao.
Sabahi: Kulitokea nini kwa duka baada ya serikali kuu ya Somalia kusambaratika mwaka 1991?
Sidow: Lilipitia nyakati ngumu sana, na kila mmoja anaweza
kufahamu matatizo ambayo yanaweza kumkabili mtu ambaye amekuwa
akifanyakazi katikati ya vurugu mjini Mogadishu bila ya kwenda popote
pengine hata kwa siku moja, Wakati ule, duka halikuwa kama lilivyo sasa;
lilikuwa dogo sana.
Nyakati nyingine tulilazimika kuchora picha nyumbani ambapo tulikuwa
hauwezi kuja dukani kutokana na mizozo. Hakukuwepo na wakati ambapo
tulisitisha kutengeneza sanaa, Tulilifanyia kazi kila tatizo na hali na
baba yangu hakuwahi kufanya kitu kingine chochote isipokuwa sanaa. Hicho
ndicho alichokijua na aliking'ang'ania.
Sabahi: Tuambie kuhusu nyakati ngumu ulizowahi kukutana nazo.
Sidow: Kila hali ina taathira zake, lakini mbaya zaidi ilikuwa
mwaka 2006 wakati Mahakama za Kiislamu zilipokuwa zinatawala sehemu
nyingi za nchi, ikiwemo Mogadishu. Wakati ule, walitulazimisha kuifunga
Studio ya sanaa ya Shik Shik, na walituambia kuwa picha tulizokuwa
tunatengeneza zilikuwa dhambi inayokatazwa katika Uislamu.
Sabahi: Mlifanya nini?
Sidow: Wakati ninaposema kuwa Studio ya Sanaa ya Shik Shik
ilifungwa, haimaanishi kuwa milango ya studio ilikuwa imefungwa kabisa.
Tulipigwa marufuku tusichore chochote na badala yake ikawa tunachora
mabango ya matangazo na matangazo ya maduka.
Sabahi: Lini mliendelea tena na uchoraji?
Sidow: Tuliendelea na ubunifu wetu wa sanaa wa kawaida mwanzoni
mwa mwaka 2007 wakati Muungano wa Mahakama za Kiislamu zilipoondoshwa na
majeshi ya Ethiopia na mfiko wa vikosi vya serikali ya mpito.
Sabahi: Kitu gani kiliwafanya mbaki nchini wakati wa vita?
Sidow: Mwenyezi Mungu ndiye anayeamua nani aondoke, na baba yetu
alikuwa sababu yetu ya kubaki nchini. Alituhamasisha kuendelea na sanaa
yetu na tubakie nchini mwetu.
Vijana wa Somalia wamekumbana na matatizo mengi wakati walipokuwa
wanajaribu kwenda nje. Wanapotea baharini kila siku. Kwa kufikiria hilo
akilini kwetu, ungekuwa upuuzi kwetu kujipeleka kwenye matatizo yote
hayo.
Sabahi: Unaionaje hali ya sasa ya Mogadishu?
Sidow: Hali ya Mogadishu inaimarika siku baada ya siku. Kwa kweli
tunafuraha sana na serikali mpya na tunatumai kuwa itaweza kufanya
mengi kuhusu hali ya usalama na kurejesha huduma za jumla za raia.
No comments:
Post a Comment