Saturday, January 26, 2013

Ubadhirifu na upotevu wa fedha shirika la umeme Zanzibar wagundulika.


 
 
 
 
 
 
Rate This

Imewekwa na Hamed Mazrouy
shehe
KAMATI YA KUCHUNGUZA NA KUDHIBITI HESABU ZA SERIKALI IMEGUNDUA UBADHIRIFU NA UPOTEVU WA FEDHA KATIKA SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR ULIOTOKANA NA UUNGWAJI WA HUDUMA YA UMEME KWA WATEJA. AKIWASILISHA RIPOTI YA KAMATI HIYO YA KUCHUNGUZA UTENDAJI WA SHIRIKA HILO MWENYEKITI WA KAMATI HIYO MH. OMAR ALI SHEHE AMESEMA UBADHIRIFU HUO UMEFANYWA NA BAADHI YA WATENDAJI WA SHIRIKA HILO KWA KUSHIRIKIANA NA WATEJA.
 AMESEMA BAADHI YA WATEJA WALIOUNGIWA HUDUMA YA UMEME HASA KISIWANI PEMBA VIWANGO VYA MALIPO HALISI VIMETOFAUTIANA NA MALIPO YALIOAINISHWA KATIKA RISITI.
AMEFAHAMISHA KUWA MIONGONI MWA UDANGANYIFU HUO NI KUGUNDUA RISITI YENYE MALIPO YA SHILINGI MILIONI MBILI NA LAKI TANO, WAKATI MALIPO ALIYOTOZWA MTEJA NI SHILINGI MILIONI 37.
MH. SHEHE AMESEMA SHIRIKA HILO PIA LIMEPOTEZA MILIONI 185 ZINAZOTOKANA NA UUNGAJI WA UMEME KATIKA MINARA YA SIMU 46 KISIWANI PEMBA .
KAMATI HIYO PIA ILIGUNDUA KUWEPO KWA AJIRA NA NAFASI ZA MASOMO ZA UPENDELEO, UTOWAJI WA UNIT ZA UMEME KUANZIA 100 HADI 800 BURE KWA WATENDAJI WA SHIRIKA HILO WAKIWEMO WAJUMBE WA BODI.
KAMATI HIYO IMEPENDEKEZA KUWAJIBISHWA KWA WAJUMBE WA BODI ILIYOPITA KUTOKANA NA KULITIA HASARA SHIRIKA LA UMEME.

No comments:

Post a Comment