Majeshi ya Somalia yalifanya operesheni katika kijiji cha Bayahow
karibu na Jowhar siku ya Alhamisi (tarehe 24 Januari) baada ya kundi la
al-Shabaab kulivamia eneo la Jowhar usiku mmoja kabla ya siku hiyo,
uliripoti mtandao wa habari wa Garowe nchini Somalia.
Hakuna mapigano yaliyoripotiwa kwenye operesheni hiyo mjini Bayahow,
lakini vikosi vya usalama vinaripotiwa kuwatia nguvuni watu kadhaa
wanaoshukiwa kuwa wanamgambo.
"Majeshi ya Somalia yamejibu mashambulizi ya al-Shabaab," alisema
Jenerali Mohamed Saney, Kamanda wa Jeshi la Somalia katika Kitengo cha
Pili. "Tunaamini kuwa mashambulizi hayo yaliandaliwa katika mji wa
Bayahow, karibu na Jowhar." Alisema kuwa mwanamgambo mmoja wa al-Shabaab
ameuawa katika uvamizi wa Jumatano.
Wakaazi wa mji huo walisema kuwa mapigano hayo yalidumu kwa muda wa
saa moja na waliona miili kati ya mitano hadi sita ya wapiganaji
waliokufa kutoka na tukio hilo. Jowhar imebakia tulivu huku Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Afrika nchini Somalia vikiendelea kuulinda mji huo.
No comments:
Post a Comment