Vijana nchini wametakiwa kufata njia za kisheria katika mfumo mzima wa utafutaji riziki katika maisha yao ya kila siku na badala yake waachane na tabia mbaya za ubakaji na wizi pamoja na matendo yote maobu kwani kufanya hivo kutaweza kupotea kwa amani na utulivu iliopo sasa hapa nchini kwetu.
Hayo yameelezwa na Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Bw,Khalfan Othman Maalim wakati alipokuwa akizungumza na Zanzibardaima huko ofisini kwake Darajani mjini unguja.
Aidha amewataka vijana wa Kizanzibar wajikite zaidi katika sekta ya kilimo kwani ndio uti wa mgongo wa taifa letu,pia amesema kufanya hivo kutaweza kuwaepusha vijana wengi kuingia katika matendo haramu yaiwemo uvutaji wa madawa ya kulevya.
Katibu huyo aliendelea kufahamisha kuwa iwapo vijana watajikita katika kilimo basi wataweza kujisaidia wawo wenyewe kwani hivi sasa suala la kilimo ndani ya Zanzibar limekuwa likifuatiliwa kwa umakini sana na viongozi wa Serikali yetu kwa lengo la kuhakikisha wanamuendeleza mkulima
Sambamba na hayo amewataka masheha kutowa vibali kwa wingi kuwapatia vijana wote ambao wana taka kujiingiza katika sekta hii ya kiilimo ili kuokoa dimbwi kubwa la vijana wasiokua na ajira hapa nchini.
No comments:
Post a Comment