Picha sio halisi
Mahakama Kuu ya Kenya hapo siku ya Alhamisi (tarehe 17 Januari) iliipa idhini Mamlaka ya Mapato ya Kenya kukusanya kodi kutoka kwa watu kadhaa, wakiwemo wabunge, ambao walikwepa kulipa huko nyuma, liliripoti gazeti la Daily Nation la Kenya.
Jaji wa Mahakama Kuu Weldon Korir alipitisha uamuzi kwamba Sheria ya Mshahara wa Bunge, ambayo inawakinga wabunge kutolipa kodi zao, imefutwa kwa utumikaji wa katiba ya mwaka 2010, inayosema kwamba wabunge lazima walipe kodi.
"Nchi hii inatokea kwenye historia ya uroho na mgawanyo mbaya wa kifedha," alisema Korir. "Fedha za umma huko nyuma hazikutumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa kwa maendeleo ya nchi na ni kwa sababu hiyo ndipo misingi ya fedha za umma ikaingizwa kwenye katiba."
Mwaka jana, makundi 18 ya haki za binaadamu yalifungua kesi ya kikatiba wakitaka mahakama itangaze kwamba maafisa wote wa nchi wanawajibika kulipa kodi. Korir alisema kwa hakika watu wote wanaofanya kazi nchini humo wana wajibu huo.
Wabunge wa Kenya wamejikuta kwenye lawama kali mwaka huu, huku wabunge waliomaliza muda wao wakipingwa kwa kujipigia kura mara mbili kujitwalia kitita kikubwa cha fedha za mafao, hatua ambazomara zote mbili zilipigiwa kura ya veto na Rais Mwai Kibaki.
No comments:
Post a Comment