Thursday, January 24, 2013

Wapiga kura wa Kenya wanakosa taarifa kuhusu wagombea wa nafasi za ndani

Zikiwa zimesalia siku chini ya 40 kabla ya uchaguzi wa tarehe 4 Machi nchini Kenya, wasiwasi unazidi kuongezeka kwamba raia wengi bado hawajui sana kuhusu wagombea wanaoshindania viti vya ndani.
  • Wakenya watapiga kura yao jijini Nairobi wakati wa uteuzi wa chama tarehe 17 Januari. Raia wengi wanasema bado hawajui kuhusu wagombea wanaoshindania viti vya ndani. [Simon Maina/AFP] Wakenya watapiga kura yao jijini Nairobi wakati wa uteuzi wa chama tarehe 17 Januari. Raia wengi wanasema bado hawajui kuhusu wagombea wanaoshindania viti vya ndani. [Simon Maina/AFP]
Wakaazi wa Nairobi wamesema kwamba wakati wakiwa wanajihisi vizuri kupata taarifa za kutosha kuhusu wagombea urais, hawana taarifa za kutosha kuhusu wagombea katika ngazi za ndani.
"Ninachanganyikiwa," alisema Anyango Auma, mwenye umri wa miaka 37, mmachinga wa mitaa ya Donholm jijini Nairobi. "Kama tunavyozungumza, Bado simjui nani anagombea nafasi ya gavana wa nchi, mjumbe wa Baraza la taifa, wawakilishi wa kina mama katika wilaya, mjumbe wa seneti au kata ya jiji."
"Yote ambayo nimekuwa nikisikia kwenye mikusanyiko mikubwa ya kisiasa na kwenye majukwaa mengine ni Raila Odinga au Uhuru Kenyatta kwa nafasi ya Urais," aliiambia Sabahi.
Waziri Mkuu Odinga ni mgombea wa urais kwa Muungano wa Mageuzi na Demokrasia, ambapo Naibu Waziri Mkuu Kenyatta ni mgombea kwa tiketi ya Muungano wa Jubilii. Wanaume hawa wawili wanachukuliwa kama washindani wakuu wa nafasi ya uraisi katika uchaguzi ujao, ambao ni wa mwanzo kuangukia kwenye mfumo wa serikali ambao unaweka nguvu kubwa katika utawala wa serikali za mitaa.

Kukosa taarifa 'mwelekeo unaoleta wasiwasi'

Chini ya usajili mpya uliotajwa na katiba ya 2010, mifumo ya serikali katika majimbo nane ya Kenya itabadilishwa na utawala wa wilaya 47 ambao utakuwa kama ngazi ya pili ya serikali baada ya mamlaka ya shirikisho.
Katika uchaguzi uliopita, Wakenya walipiga kura tu kumchagua rais, wabunge na madiwani (wawakilishi wa kata). Mwezi Machi, Wakenya watapigia kura nafasi sita za uchaguzi: rais, maseneta, magavana wa majimbo, wabunge, wawakilishi wa majimbo wa raia na wanawake.
Alex Mung'aro, mhasibu jijini Nairobi, alisema hakushiriki katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vya siasa wiki iliyopita kwa sababu hakuwa na taarifa za kutosha.
"Bosi wetu alitupa siku moja ya mapumziko ili tuweze kushiriki katika uteuzi wa vyama, lakini sikushiriki kwa sababu sikua najua [wagombea ni akina nani] wanaotafuta 'tiketi' za chama," aliiambia Sabahi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Demokrasia Peter Aling'o aliuita ukosefu wa taarifa miongoni mwa wapiga kura ni "mwelekeo unaoleta wasiwasi".
"Inaogopesha sana kwa sababu mpiga kura asiye na taarifa wakati wote atatoa uamuzi usio wa busara, ambao una madhara kwa demokrasia na utawala bora," aliiambia Sabahi. "Inaleta hatari kwa mafanikio mazuri ambayo serikali husika iliahidi kuleta nchini Kenya."
Aling'o alivilaumu vyombo vya habari na taasisi za serikali kwa kushindwa kuuelimisha umma kuhusu madaraka ya kikatiba ya kugatua madaraka ya serikali.
"Vyombo vya habari vimekuwa vikijazwa habari zinazowalenga wagombea wa urais -- Odinga na Kenyatta. Vimepunguza kila kitu kwa ajili ya watu wawili, na kufanya ionekane kama uchaguzi unahusu urais tu," ailsema. "Kwa upande mwingine, chombo cha uchaguzi na vyama vya siasa vimeshindwa kuendesha elimu ya kutosha ya mpiga kura ili kuwawezesha raia katika jukumu lao."
Adams Oloo, mhadhiri wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Nairobi, alisema isipokuwa kama Wakenya wakiwa wamejiandaa kwa uelewa kuhusu wagombea, siku ya uchaguzi itakuwa "ya kuudhi".
"Hii ni mara ya kwanza Wakenya wanashiriki katika zoezi gumu la kupiga kura, lakini hawakuandaliwa vizuri mapema, hivyo wanaweza kukosea," aliiambia Sabahi. "Kuenda katika uchaguzi wakati hujui ni nani unayekwenda kumpigia kura kutawafanya wapigakura kuwapigia kura watu wasiowajua."
"Lakini bado hazijapotea," alisema. "Kama elimu ya mpigakura kwa umma [kampeni] imezinduliwa nchi nzima katika siku chache zilizobaki, nina uhakika Wakenya watajifunza jinsi ya kushiriki."

IEBC: Hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi

Ofisa mtendaji mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) James Oswago pia alisema hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.
Alisema IEBC inatoa elimu ya mpigakura kwa hatua kuepuka kuujaza umma na taarifa nyingi kupita kiasi.
"Hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi," aliiambia Sabahi. "Mwezi Novemba mwaka jana, elimu yetu ya mpigakura ililenga katika kuuhimiza umma kujiandikisha kama wapigakura. Wiki hili na sehemu ya wiki lijalo, ujumbe wetu umelenga katika kuwashawishi kuhakiki hali ya uandikishwaji kabla ya kuwaletea elimu kamili ya nafasi zilizogombewa na wajibu wa nafasi zote zinazofanyiwa uchaguzi."
Alihadharisha, hata hivyo, elimu hiyo ya mpigakura sio wajibu pekee wa IEBC, lakini unapaswa pia kufanywa na vyama vya siasa na vikundi vya kiraia.
Tarehe 4 Machi, Wakenya watachagua wagombea kwa ajili ya nafasi 1,882 zilizogombewa: wabunge nafasi 290, maseneta nafasi 47, magavana wa majimbo 47, wanawake wawakilishi wa majimbo 47, wawakilishi wa wananchi katika kata 1,450 na urais.

No comments:

Post a Comment