Friday, January 25, 2013

Zanzibar inania ya kuekeza zaidi katika secta ya utalii Waziri Aboud


 
 
 
 
 
 
Rate This

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Muhamed akizungumza na ujumbe wa Kampuni inayo shuhulikia Ujenzi na Uchumi wa nje(ANHU)Group co,LTD ya China kulia yake ni Makamo wa Rais wa Kampuni hiyo Wang Hao,huko ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Muhamed akizungumza na ujumbe wa Kampuni inayo shuhulikia Ujenzi na Uchumi wa nje(ANHU)Group co,LTD ya China kulia yake ni Makamo wa Rais wa Kampuni hiyo Wang Hao,huko ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa  Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amesema kuwa kuekeza katika shopping more itakuwa kivutio kikubwa  kwa  watu mbali mbali na kuweza kukuza uchumi  nakuondokana na umasikini nchini.

Aliyasema hayo  huko katika Ofisini  kwake vunga Zanzibari wakati akiwa na mazungumzo na kampuni ya (ANHU)Group co,LTD ya China.

Aidha alisema kuwa Zanzíbar inania ya kuekeza katika sekta ya utalii kwani  sekta hiyo ndiyo inayoweza kukuza uchumi wa nchi .

Alieleza kuwa waekezaji hao wataweza kuekeza Zanzíbar mpaka waweze kufanya utafiti wa maeneo ambayo wanatarajia kuekeza ili waweze kuridhika nayo kwa biashara .

Waziri huyo amesema kuwa kampuni hiyo imeweza kuekeza sehemu Mbali Mbali za kimataifa pamoja  na África mashariki ikiwemo Zimbabwe na Muzambiq.

Alifahamisha kuwa katika nchi yetu ya Zanzíbar tunategemea zaidi uchumi wetu kwa  njia ya utalii ikiwa  wawekezaji  wa kampuni hiyo wataekeza wataisaidia serikali kuengeza pato kutokana na kivutio kwa kitalii.
“Utalii ni kiungo kikubwa kwa serikali” alisema Abuod.

Alisema kuwa kampuni mbali mbali ambazo zinataka kuekeza Zanzíbar kwa kushajihisha maeneo mengine  tofauti Serikali haina pingamizi kwani inaunga mkono jitihada za Serikali.

Pia alifahamisha iwapo wawekezaji wataekeza Zanzíbar wananchi watafaidika kwa kuweza kupata ajira nchini mwao .

No comments:

Post a Comment