Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, Fowsiyo
Yusuf Haji Aadan, alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza
William Hague mjini London siku ya Alhamisi (tarehe 3 Januari)
kujadiliana maendeleo nchini Somalia.
"Somalia imepiga hatua zinazoonekana za maendeleo kwenye miezi ya
karibuni, kisiasa kufuatia kumalizika kwa kipindi cha mpito na katika
kuimarisha usalama, huku al-Shabaab wakifukuzwa kwenye miji mikubwa. Ni
jambo muhimu kwamba kasi hii iendelee," alisema Hague kwenye taarifa kwa
vyombo vya habari.
Hague alisema Aadan alizungumzia mipango ya serikali ya Somalia
kuimarisha usalama, kuongeza fursa za upatikanaji haki na kupigania
utawala wenye uwazi kwenye masuala ya fedha, muafaka wa kisiasa na
maendeleo ya kiuchumi. "Uingereza imedhamiria kushirikiana na serikali
ya Somalia kusaidia vipaumbele hivi na kuhakikisha msaada wa pamoja wa
kimataifa," alisema.
Aadan anatarajiwa kuzitembelea nchi nyengine kadhaa wiki hii kurekodi fedha za Somalia kwenye benki za kigeni.
Aadan alisema mkutano wake na Hague ulikuwa na "manufaa", kwa mujibu wa ukurasa wake wa Twitter.
No comments:
Post a Comment