Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia imetangaza mpango wa kuratibu na
kufanya hifadhi yake ya nyaraka kuwa ya kisasa, ambayo iliepuka
majaribio kadhaa ya kutaka kuporwa na kuharibiwa kwa kipindi cha miongo
miwili iliyopita.
Sheikh Ahmed Nur, mkurugenzi wa idara ya utawala na fedha ya wizara,
alisema wizara hiyo inapanga kutathmini ukamilifu wa nyaraka zake za
siri, ikiwa ni pamoja na mikataba na mapatano ambayo yanahusiana na
kiwanda, jeshi, ushirikiano wa sayansi na teknolojia.
"Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia na Ushirikiano wa Kimataifa
unaangalia namna ya kuhuisha uhusiano wa kidiplomasia na jumuiya za
kimataifa katika namna ambayo inatofautiana na serikali za mpito
zilizopita ambazo ziliitawala nchi kwa mafanikio baada ya kuanguka kwa
serikali kuu ya kijeshi iliyotawala kwa miaka 22 iliyopita," Nur
aliiambia Sabahi.
"Hifadhi zetu ya nyaraka za taifa zitaweza kutupa taarifa na mwongozo
kuhusu mapatano yaliyopita na deni lililobakia la Somalia, na pia akaunti za benki za nje za Somalia na mali, ambazo zinajumuisha maeneo ya biashara na majengo ya balozi na balozi ndogo,"
alisema. "Hii itatoa taarifa muhimu kwa wafanya uamuzi katika wizara
pamoja na watafiti na wataalamu wa nyanja mbalimbali, hususani uhusiano
wa kimataifa."
Nur alisema asasi ya hifadhi za nyaraka itashirikiana na uundaji mpya
mkubwa wa wizara, ikiwa ni pamoja na mradi wa kisasa ili kuziwekea
ofisi zake kompyuta, upatikanaji wa intaneti, kamera za uchunguzi, skana
za utambuzi kwa wafanyakazi wa wizara, vifaa vya elimu ya lugha na
masomo ya kidiplomasia, na majenereta ya umeme.
Mwanadiplomasia mstaafu Abubakar Adow, mshauri wa Wizara ya Mambo ya
Nje, alisema mradi huo mpya utasaidia wizara wakati inajitayarisha
kubadilisha upya muundo wa wafanyakazi wake nchini Somalia na ujumbe wa
kidiplomasia nchi za nje.
"Tuna fursa ya kweli," aliiambia Sabahi. "[Kwa msaada wa fedha
kutoka] serikali rafiki na mashirika ya maendeleo, waziri wa mambo ya
Nje na Ushirikiano wa kimataifa anaweza kuwa na hifadhi pana ya nyaraka
inayozingatia viwango vya sasa vya kimataifa na vigezo, hivyo
kuhakikisha utunzaji wa nyaraka ili zisiharibike au kupotea."
Adow alisema wizara inataka kuunda idara ya hifadhi kuu ya nyaraka
ili kuandaa na kuweka katika dijiti makala za kihistoria na kuajiri na
kuwafundisha wafanyakazi kusimamia kumbukumbu.
Polisi Abdi Mohamed Samatar, ambaye ni kiongozi wa kitengo ambacho
kinalinda wizara, alisema yeye na wanajeshi wengine wawili wamefanya
kazi tangu miaka ya 1980 kulinda hifadhi ya nyaraka.
"Wanamgambo hutufyatulia risasi wakitumia bunduki zao za rashasha,"
aliiambia Sabahi. "Wakati wa tukio hilo mwezi Aprili 1995, nilipigwa
risasi na ilibidi nikae katika Hospitali ya Medina, ambayo iko karibu na
wizara, kwa siku 25 kabla ya kuodoka."
Kitengo kidogo cha Samatar pia kilipambana mara kadhaa na wanamgambo
wa kikabila kutaka kuchukua majengo ya wizara na kuyageuza nyumba za
kuishi au maduka ya biashara. "Tumekuwa makini sana kuhusu shughuli hizo
ambazo si kwa maslahi ya umma," alisema.
Samatar alisema Muungano wa Mahakama za Kiislamu (ICU) ulichukua
jengo la Wizara ya Mambo ya Nje mwaka 2006 na kuondoa hifadhi za nyaraka
na kuyagawa majengo ya wizara. Wanaharakati walizuia misheni hiyo, hata
hivyo, kwa kuishawishi ICU kwamba hifadhi ya nyaraka inatoa kumbukumbu
za kihistoria kwa vizazi vijavyo.
No comments:
Post a Comment