Imewekwa na Mhamed Khamis
Mandhari ya Mji wa Wete kisiwani Pemba
Hayo yamekuja kufuatia Afisa Mdhamini na Mawasiliano kisiwana Pemba Bwana Hamadi Ahmed Baucha kuvamiwa usiku wa kuamkia jana na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi huko nyumbani kwake kifumbika Wete Pemba.
Afisa huyo amesema kuwa watu hao waliokuwa na Mapanga walivamia na kumjeruhi zsehemu kadhaaa ndani ya mwili wake ikiwemo kwenye mgongo lakini kw hawakufanikiwa kupata lolote ndani ya Nyumba hio.
Aidha amesema licha ya kupata majeraha kadhaa lakini hali yake ka sasa inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya Wete.
Kwa upande wake kamabda a Polisi kaskazini Pemba Bwana Yahya Rashid Bugi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameiomba jamii kutoa ushirikiano ipasavo pale wanapowaona watu wasiowajua ndani ya jamii zao ili hatuwa za uchunguzi zichukuliwe juu yao kwani hwenda ikawa ndio miongini mwa wanaofanya matendo mabaya
No comments:
Post a Comment