.
Kufuatia tukio la kuuwawa kwa Padri Muche kwa kupiigwa Risasi huko
Mtoni Zanzibar wakati akiwa kwenye harakati za kuhudhuria katika ibada
ya misa Chama cha Wananchi CUF kimelaani vikali kitendo hicho n cha
kiyama kwani ni kinyume na ubinadamu
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari uenezi na mawasiliano ya
Umma MH: Salim Biman kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama hicho Pr ,Ibrahim
haruna Lipumba kutokana na kuchukizwa vikali na tukiuo la kinyama
lililofanywa na baadhi ya watu wachache wenye nia mbaya na Nchi ya
Zanzibar.
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF,Professa Ibraim Lipumba
Kutokana na tukio hilo Chama cha wananchi Cuf kupitia Mkurugenzi wa habari wa chama hicho imemelitaka Jeshi la Polisi Nchini kuwa makini na matukio ya kiuhalifu yanayotokea siku hadi siku ambayo yanatowa taaswira mbaya kwa wananchi wenyewe na wageni wanaokuja kutoka nje.
Pia amelitaka jeshi hilo kwa kushirikiana na Usalama wa Taifa kuendesha uchunguzi wa kina na waharaka ili kuhakikisha litawatia mbaroni wahusika wote wa tukio hili ili kuinusuru Nchi kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hivyo ametoa pole kwa waumini wa dini ya kikirsto na kuwataka wawe na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu kwao nawawe watulivu suala hili waiachie mamlaka husika kulipatia ufumbuzi wa tatizo hili.
Mh Bimani pia amewataka wanachi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha linawafichuwa wahalifu wote badal ya kuhifadhiwa kwani ni wahujumu wa taifa.
Chama cha wananchi kinaimani kuwa,wananchi waliowengi wamepatwa na huzuni pamoja na mshituko mkubwa mkubwa kufuatia tukio hilo,hivyo hali hiyo inwakosesha raha na imani ya kuishi kama ilivyo zamani.
No comments:
Post a Comment