Monday, February 18, 2013

Mafundi wa kigeni watekwa nyara Nigeria

Watu waliokuwa na silaha katika jimbo la Bauchi, kaskazini mwa Nigeria, wamewateka nyara mafundi wa ujenzi saba kutoka nchi za nje.
Ramani ya Nigeria na jimbo la Bauchi
Mlinzi katika kampuni hiyo ya ujenzi, Septraco, inayomilikiwa na Walibnan, alipigwa risasi na kuuwawa kwenye uwa wa kampuni hiyo.
Wafanyakazi kutoka Utaliana, Ufilipino, Uingereza, Uguriki na Libnan inasemekana ni kati ya wale waliotekwa nyara.
Kabla ya hapo kituo cha polisi katika mji wa Jama'are kiliingiliwa.
Polisi wa Nigeria hawakuweza kutambua waliofanya shambulio hilo lakini waandishi wa habari wanasema wanaoshukiwa ni kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram.

No comments:

Post a Comment