Jenerali Abdullahi Ali Osman, kamanda wa kikosi kikubwa cha pili cha jeshi chenye kuhusika na kukomboa maeneo ya kusini magharibi ikiwa ni pamoja na Shabelle ya chini, Bay na Bakol, Gedo, Juba ya kati, na Juba ya chini, waliwapa wavamizi wa kambi za askari na IDPs siku 30 kurudi kwenye makaazi yao ya asili.
"Tutalazimisha njia yetu kuwa makaazi yasiyo halali kisheria isipokuwa watafuata amri yetu na tutamzuia yeyote atakayeonyesha kupinga au kuharibu hali ya usalama," Osman aliiambia Sabahi.
Jeshi la Somalia kwa sasa linashikilia maeneo mawili ya Kahda na al-Jazeera katika sehemu za mji mkuu za kusini ya magharibi, wakati zilizokuwa kambi zao za askari zinashikiliwa na wafanyabiashara wa ndani wenye silaha na IDPs.
"Ningependa kuwaambia kuwa inatosha baada ya miaka 21 ya kutumia faida ya taasisi za nchi," alisema." Kila raia wa Somalia ajue kuwa jeshi litashughulikia kikamilifu waliochukua majengo yao."
Osman alisema serikali inapanga kujenga tena hospitali za jeshi huko Hodan, uwanja wa ndege wa jeshi ulio mkabala na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde, old Circolo Ufficiale, kituo cha burudani cha maofisa wa jeshi kilichopo Howlwadag, na maeneo mengine ya jeshi katika wilaya za Hodan na Daynile huko Mogadishu.
Nchi rafiki zinaisaidia Somalia kujenga makambi hayo ya mafunzo na marekebisho kwa ajili ya vikosi vya Somalia, na majengo mengine ya vifaa kama vile kiwanda kipya cha kushona sare za jeshi zinazovaliwa na maofisa na kiwanda cha vyakula vya makopo mahususi kwa wafanyakazi wa vikosi vya jeshi, Osman alisema.
Mkuu wa jeshi la Somalia Abdikadir Sheikh Ali Diini aliwataka wapiganaji wa al-Shabaab kujisalimisha, ili vikosi vya jeshi viweze kuzingatia katika kujenga upya makambi ya jeshi kwa kushirikiana na nchi washirika kwa madhumuni ya mafunzo na kuvipa vikosi zana.
"Hatutaki kuwaua vijana wetu wa kiume wote ambao wanapigana kwa jina la al-Shabaab, kundi ambalo linachafua Uislamu," alisema.
"Sasa hivi tuko katika hali ya vita dhidi ya kuvamiwa na magaidi wa al-Qaida na washirika wao Wasomali ambao wamepotea," aliiambia Sabahi. "Tunapambana na adui kwa mkono mmoja wakati tunajenga upya majengo ya jeshi letu na mkono mwingine."
Nchi washirika zaongeza msaada kwa vikosi vya Somalia
Katika miezi miwili iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia Fowsiyo Yusuf Haji Aadan na Waziri wa Ulinzi Abdihakim Haji Mohamud Fiqi wamekuwa na kazi ya kukutana na viongozi wa kigeni ili kupata fedha na kusaidia maendeleo na ulinzi.Aadan alipata msaada wa Italia katika sekta za mahakama, ulinzi na maendeleo baada ya kukutana Roma na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Giulio Terzi di Sant'Agata tarehe 7 Januari.
Somalia pia ilitia saini makubaliano ya kijeshi na Uturuki tarehe 6 Disemba ili kuimarisha ushirikiano ambao ungesaidia jeshi la Somalia na kuongeza uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Katika taarifa kwa Redio Uturuki na Shirika la Televisheni tarehe 19 Januari, Fiqi alisema maofisa 120 wa Somalia na masajenti watapata mafunzo nchini Uturuki mwaka huu.
"Usalama ni kipaumbele chetu na kikundi cha al-Shabaab cha Somalia sio tu tishio kwa wenyeji, lakini ni tishio la kimataifa pia," alisema. "Ni muhimu kwa jamii ya kimataifa kutoa msaada hadi tutakapokuwa na uwezo kusimama kwa miguu yetu wenyewe."
Msaada zaidi wa kurejesha amani na usalama nchini Somalia, Waziri wa Maendeleo wa Uturuki Cevdet Yilmaz tarehe 27 Januari aliwasilisha hundi ya dola milioni 1 kutoka katika serikali ya Uturuki kwa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Kuwaandaa wanajeshi wa Somali kuendelea na usalama
Mukhtar Osman Roraye, mtaalamu wa masuala ya jeshi wa Somalia, alisema maofisa wa Ulaya kutoka Hispania, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji na Uholanzi wanatoa mafunzo kwa mamia ya wanajeshi wa Somalia katika kambi ya jeshi karibu na Kampala, Uganda. Serikali ya Sudan na Ethiopia pia wana wajibu wa muhimu katika kuwafundisha wanajeshi na polisi kujibu mapigo kwa wapiganaji ambao wanajihusisha na mbinu za vita vya msituni, alisema.Baada ya Baraza la Umoja wa nchi za Ulaya kuongeza muda wa zoezi lake la mafunzo kwa wanajeshi wa Somalia kwa miaka miwili zaidi tarehe 22 Januari, Zoezi la Mafunzo la Umoja wa nchi za Ulaya (EUTM) nchini Somalia lilisema "litaendelea kuchangia kuimarisha jeshi la Somalia ili waweze kuendeleza wajibu wa usalama".
Karibia wanajeshi 3,000 wa Somalia wamekuwa wakifundishwa chini ya EUTM Somalia tangia uzinduzi wake mwezi Februari 2010.
Roraye alisema nchi marafiki zitaweza kuchangia vifaa vya kisasa vya kijeshi kwa jeshi la Somalia kama Umoja wa Mataifa utaamua kuisaidia vikwazo vya kijeshi viliwekwa kwa Somalia tangia mwaka 1992.
"Kwa sababu ya msimamo na malengo yake, jeshi la Somalia, ambalo halimiliki matengi, mota, vifaru na sare, linapigana dhidi ya maadui wahalifu ambao wanataka kuharibu na kuwafanyia ugaidi watu wake na wananchi wote wa nchi za Afrika Mashariki hususan Kenya, Ethiopia, Uganda na Burundi," Roraye aliiambia Sabahi.
No comments:
Post a Comment