Monday, February 4, 2013

Jeshi la Ufaransa lalenga ngome za waasi

 4 Februari, 2013 - Saa 12:41 GMT
Ndege za jeshi la Ufaransa zimekuwa zikishambulia ngome za wapiganaji kwa lengo la kuziba maeneo wanayotumia kusafirishia silaha zao
UfaNdege za kijeshi za Ufaransa, zimeshambulia kwa mabomu ngome za wapiganaji na maghala yao ya silaha katika maeneo ya vijijini ili kujaribu kukata njia wanazopitishia silaha zao.
Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Laurent Fabius, waasi hao hawatweza kuendelea kupigana bila kupata chakula na silaha wanazohitaji.

Ndege 30 za kijeshi, zilifanya mashambulizi siku ya Jumapili, latika eneo la Tessalit huku kukiwa na hofu, kuwa wapiganaji hao huenda wakajipanga upya
Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa bei ya chakula na mafuta imepanda sana huku baadhi ya wafanya iashara wakitoroka kwa hofu ya kushambuliwa.

No comments:

Post a Comment